Habari za Punde

Kampuni ya Ndege ya Precision yazindua Safari Zake Kisiwani Pemba leo.

Ndege ya Kampuni ya Precision Air, ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Karume Pemba ikiwa ni Uzinduzi wa Safari zake kisiwani Pemba, ikipokelewa na Kikosi cha ZimaMoto kwa kumwagiwa maji kuashiria kuipokea Ndege hiyo na kuanza safari zake rasmin kisiwani huo. 

Ndege ya Kampuni ya Precision Air ikiwa katika Uwanja wa Ndege Kurume Kisiwani Pemba kwa ajili ya Uzinduzi wa Safari zake Pemba. kurahisisha usafiri kwa Wananchi wa Zanzibar na Nchi jirani.Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba,Mhe.Mwanajuma Majid Abdalla, akihutubia wakati wa uzinduzi wa safari za ndege ya Precision Air uliofanyika katika Uwanja wa Karume Pemba.

Mkuu wa Mkoa Kusini Pemba Mhe.Mwanajuma Majid Abdalla, akikata Utepe kuashiria uzinduzi wa safari za Ndege ya Kampuni ya Precision Air kisiwani Pemba wakati wa uzinduzi wa safari za ndege hiyo kwa kutowa huduma za usafiri kwa Wananchi wa Visiwa vya Pemba Unguja na Tanzania Bara. 
Mkuu wa Mkoa Kusini Pemba,Mhe.Mwanajuma Majid Abdalla,akilishwa keki baada ya uzinduzi wa safari za ndege za Kampuni ya Precision Air kisiwani Pemba.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe Mwanajuma Majid Abdalla,akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Kampuni ya Precision Air wakati wa uzinduzi wa Safari za ndege hiyo kisiwani Pemba, uliofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Karume Pemba

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.