Habari za Punde

Mambo matano ya kuzuia Kipindupindu


1. Maji ya kunywa na ya kutumia.

Hakikisha kama kuna uwezo kupata maji ya chupa ilio na seal nzima. Hakikisha unanunua katika maduka ya uhakika badala ya vichochoroni. Tumeona viwanda vya majumbani vya wachina wanaouza maji katika chupa tena zilizo na seal lakini hayako salama. Nunua katika maduka unayoyaamini badala ya wafanyabiashara wasio waaminifu.

Kama huna uwezo basi chemsha maji mpaka yachemke halafu uyawache yapoe ndio utumie. 
Vile vile unaweza kutumia drops mbili za bleach katika kila lita moja ya maji , ya kukoga na matumizi mengine mwilini. Bleach ni disinfectant inayoua vijidudu. Ushauri huu hutolewa kwa wanafunzi wanapotembelea sehemu zilizoathirika na maradhi kama haya. Hakikisha maji hayo ndio unayotumia kuogea, kupiga msuaki na matumizi mengine. Hata barafu nayo ni vyema ikatengenezwa kwa maji yaliochemshwa.
Hakikisha unakosha sehemu unayotumia kupikia chakula kwa maji na sabuni na kuwacha mpaka pakauke kabla ya kutumia tena sehemu husika.
2. Kosha mikono yako

Kabla ya kula na baada ya kula (au kabla ya kumtayarishia mtoto chakula) hakikisha unaosha mikono kwa sabuni na kuhakikisha unasafisha mpaka kuliko katika ncha za kucha. 

Ukoshaji wa mikono unatakiwa uanzie kwenye matumbo ya viganja, juu ya viganja, katikati ya vidole, na katika kucha, kipindi hichi si cha kufuga kucha refu.

Kosha mikono yako kwa sabuni baada ya kutumia choo, na hakikisha unafika hadi katikati ya vidole na ncha za kucha. Vile vile baada ya kumsafisha mtoto ni lazima ukoshe mikono yako kwa sabuni.
Kama kuna mgonjwa wa kipundupindu basi hakikisha unakosha mikono yako mara kwa mara hasa unapomsafisha.
3. Hakikisha usafi katika vyoo na ikiwezekana tumia bleach kidogo alau mara mbili kwa siku kuanzia katika sakafu ya vyooni, sehemu za kukalia safisha kwa sabuni kabla ya matumizi usiwache uchafu ukatapakaza maradhi. 
Siri hapa ni kusafisha na kuhakikisha kunakauka ikiwezekana kabla ya matumizi. Tumia 10ml za bleach kwa kila lita moja ya maji katika kusafisha. Hii ni kwa ajili ya kusafisha tu, bleach ni sehemu moja katika 9 ya maji katika kuchanganya.

Kwa wasio na vyoo, basi hakikisha unafanya haja mbali na vyanzo vya maji, na unafukia baada ya haja katika shimo la urefu wa kutosha. Inasikitisha kutoa ushauri huu katika dunia ya leo kwamba kuna baadhi ya wananchi hawana vyoo majumbani.
4. Pika chakula vizuri 

Hakikisha chakula kinapikwa vizuri katika moto mpaka kitokote. Kipindi hichi si cha kuchaguwa nyama iliokuwa  imepikwa nusunusu (half cooked). Hakikisha kinapikika vizuri hasa samaki, na nyama, kifunike muda wote,na kula wakati kimoto, na hakikisha kama ni mlaji wa matunda basi yamenye na kuyakosha vizuri kabla ya kula.

5. Kwa nyumba ilioathirika na  kipindup[indu (cholera)

Hakikisha unafuata kinga nne hapo juu kwa wakati wote kuzuia kusambaza maradhi kwa wengine na vile vile uweze kujilinda mwenyewe na maradhi.

Tumia rubber globes ikiwezekana katika kusafisha sehemu aliopo mgonjwa. 
Hakikisha unakosha  mashuka (bedding) ya mgonjwa, chumba na hata sakafu kwa maji ya moto na bleach ili kuzuia kusambaza maradhi. 
Kama umekusudia kuyatupa magodoro na matandiko hakikisha yamefungiwa vizuri na wapewe wahusika wa masuala ya taka kuja kuyaondoa, au ikiwezekana yakoshe kwanza kabla kuyatupa. Tumia bleach ya kawaida 10ml kwa kila lita moja ya maji ya kuchanganya kwa ajili ya kusafishia, 
Tumia maji ya moto na hakikisha huchanganyi nguo za mgonjwa na wengine walio wazima.
Ilivyo hutakiwi kumkaribisha chakula mtu mwengine asieishi katika nyumba yako ikiwa nyumba yako tayari ina mgonjwa alieathirika na kipindupindu. 
Kipindi hichi si cha kula vijumbani, majiani au mikahawani, ni jitihada za kuzuia kusambaa kwa maradhi. 
Vile vile mgonjwa wa kipindupindu haruhusiwi kuogelea katika swimming pool au kwenye mito na hata baharini mpaka wiki mbili baada ya kuhakikishiwa kuondoka kwa maradhi.
Ikiwa usafi utadumishwa na kuwekewa jitihada za kweli basi kipindupindu hakiwezi kuwa na athari kubwa. Ni suala la usafi hasa katika matumizi ya maji, upishi na mazingira ya majumbani mwetu.
Kwa hisani ya mdau kutoka Face Book

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.