Habari za Punde

Mwenge wa Uhuru waingia Mkoa wa Mjini Magharibi baada ya kumaliza mbio zake Mkoa wa Kaskazini

 Mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja Meja Mstafu. Juma Kasim Tindwa akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis tayari kwa kukimbizwa katika mkoa huo.
 Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Magharibi A, Mwinyiussi Abdalla kwa ajili ya kukimbizwa katika Wilaya yake.
 Mkuu wa Wilaya ya Magharibi A, Mwinyiussi Abdalla akiteta kitu na kiongozi wa mbio za Mwenge 2016 George Jackson Mbijima wakati wa sherehe za makabidhia ya Mwenge yaliyofanyika Mfenesini Wilaya ya Magharibi A.
Mmoja wa wakimbiza Mwenge wa Uhuru mwaka 2016 James Sadick Munguji akiongoza  mbio hizo katika mitaa ya Mfenesini, Wilaya ya Magharibi A.

 Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.