Habari za Punde

Taasisi ya Sayansi za Bahario yaadhimisha wiki ya Tafiti Zanzibar


Mkurugenzi wa Taasisi ya Sayansi za Bahari Zanzibar (IMS) Dkt. Yohana Shaghudi akisoma risala wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya utafiti yaliyofanyika Ofisi za Taasisi hiyo Malindi Mjini Zanzibar.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kamisheni ya Sayansi na Teknolojia Tanzania Dkt. Hassan Mshinda akifungua wiki ya maadhimisho ya utafiti yaliyofanyika Ofisi ya IMS Malindi Mjini Zanzibar.
 Mkurugenzi Mshiriki Dkt. Matern Mtolera akiwasilisha moja ya tafiti zilizofanywa na Taasisi ya Sayansi za Bahari wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya utafiti yaliyofanyika Ofisi za Taasisi hiyo Malindi Mjini Zanzibar.
 Mwanasayansi mwandamizi wa Taasisi ya Sayansi za Bahari DKT. Mohammed Maalim akiwasilisha utafiti wa takataka kugeuzwa mbolea kwa ajili ya kuimarisha mazao ya kilimo mashambani.

Mgeni rasmi Dkt. Hassan Mshinda (wa katikati) waliokaa katika picha ya pamoja ya washiriki mkutano wa maadhimisho ya wiki ya utafiti yaliyofanyika Ofisi ya IMS Malindi Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

Khadija  Khamis  na Maryam  Kidiko  - Maelezo 
.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknologia Tanzania  Dkt Hassan Mshinda alisema Taasisi ya Utafiti wa  Sayansi za Bahari Zanzibar (IMS) imetoa mchango  mkubwa  katika  kuimarisha Uchumi  wa Zanzibar.

Amesema Utafiti wa zao la mwani ambao umefanywa na Taasisi hiyo umekuwa mkombozi kwa wanawake wengi wa Zanzibar hasa wanaoishi kando kando ya bahari ya Visiwa hivyo.

Dkt Mshinda aliaeleza  hayo alipokuwa   akifungua maadhimisho ya wiki ya utafiti katika Taasisi ya Sayansi za Bahari ya Chuo Kikuu cha Dar-es-salam iliopo  Malindi Mjini Zanzibar .


Amesema zao la mwani hivi sasa linashika nafasi ya tatu katika kuingiza fedha za kigeni Zanzibar, ikitanguliwa na zao la karafuu na sekta ya utalii,  na iwapo juhudi zitaendelezwa   kunadalili miaka michache ijayo mwani ukachukua  nafasi ya  kwanza.

Ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kwa mwamko wake wa  kuanzisha vitengo vya utafiti katika Wizara zote ikiwa na lengo la kushajiisha kufanyika tafiti mbali mbali na matokeo ya tafiti hizo kutumika katika kutekeleza sera kwa ajili ya maendeleo yake.

Alisema kuwa tafiti nyingi zinazofanyika nchini huchangia kukuza uchumi wa nchi na kupunguza umasikini kwa  kuzalisha ajira nyingi  zisizo rasmi  hasa kwa vijana.

Alifahamisha kuwa  lengo la Vyuo Vikuu  pamoja na kufundisha wanafunzi pia vinajukumu  la kufanya tafiti   mbali mbali ambazo  matokeo ya tafiti hizo yatatumika vizuri  yananafasi kubwa yakuleta mabadiliko.

Dkt  Mshinda aliishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mchango mkubwa katika maendeleo ya Taasisi ya hiyo ikiwemo kuwapatia  eneo la ardhi lenye ukubwa wa ekari 125  katika kijiji cha Buyu na  hatua ya kuliendeleza eneo hilo zinaendelea.

Nae Mkurugenzi wa  Taasisi ya Sayansi za Bahari Dkt. Yohana Shaghude alisema Taasisi hiyo imepewa majukumu makubwa ya kufanya utafiti wa sayansi katika fani zote za bahari pamoja na kutowa ushauri bora wa matumizi ya bahari

Alisema lengo la kufanya tafiti  za aina hiyo ni kutoa elimu pamoja na ushauri  kwa wananchi  jinsi ya njia bora ya matumizi endelevu ya rasilimali zilzopo.

Aliongeza kuwa  tafiti zilizofanywa na Taasisi zimesaidia kudhibiti maeneo ya mwambao  wa bahari , uimarishaji na ubunifu wa uendelezaji wa ufugaji wa chaza pamoja na uhifadhi wa   matumbawe na mikoko.

“Taasisi ya sayansi ya bahari inajitahidi kulinda vizuri mazingira ya bahari na uendelezaji mzuri wa nishati katika bahari kama vile Mwani, Chaza,Samaki na Matumbawe” alisema Dkt Yohana.

Taasisi ya Sayansi za Bahari  Zanzibar ilanzishwa Octoba 17 mwaka 78 ikiwa imeanza na wanataaluma  sita na hivi sasa inatoa shahada za uzamivu na uzamili ikiwa chini ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.