Habari za Punde

Kikao cha kwanza kati ya Balozi Seif na Mawaziri, Manaibu Waziri wa Serikali

 Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wa kwanza kutoka kushoto akiwa pamoja na Mawaziri na Manaibu Mawaziri wa SMZ katika Kikao cha kwanza tokea wateuliwe kushika nyadhifa zao kwenye ukumbi wa Ofisi yake iliyopoVuga Mjini Zanzibar.

Wa kwanza kutoka kushoto ya Balozi Seif ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria na Utumishi wa Umma Mh. Haroun Ali Suleiman, Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali, Waziri wa Kilimo, Mali asili, Mifugo na Uvuvi Mh. Hamad Rashid Mohammed, Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Khalid Salum Mohammed,Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh. Riziki Pembe Juma na Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi Mh. Ali Juma Khatib.
 Baadhi ya Mawaziri wa SMZ wakiwa katika kikao cha pamoja na Mtendaji Mkuu wa Serikali Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hayupo pichani.

Wa kwanza kutoka kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed Aboud Mohammed, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Balozi Ali Abeid Aman Karume, Waziri wa Kazi, uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Mh. Modeline Castico, Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Mh. Salama Aboud Talib, Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Rashid Ali Juma, Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi Mh. Said Soud pamoja na Waziri wa Afya Mh. Mahmoud Thabit Kombo.

Picha na – OMPR – ZNZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.