Na Fahadi Siraji,
Same
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umesema mambo yote
yanayofanywa na Rais Dk John Magufuli tokea ashike madaraka anatekeleza
misingi ya sera, shabaha na malengo yatokanayo na ilani ya uchaguzi
ya CCM ya mwaka 2015/2020.
Imeelezwa kuwa kamwe baba hatelezi mambo yafanywayo aidha hayakutoka
mbinguni au kwenye mwezi bali yanayofanywa na serikali yake ni maelekezo
ya kisera yatokanayo na umakini wa CCM.
Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka ameeleza hayo jana katika
mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika katika eneo la Stendi Kubwa
Wilayani Same Mashariki.
Shaka alisema kasi ya
utendaji mahiri wa serikali ya Rais Dk Magufuli si nguvu ya soda kwasababu Chama
Cha Mapinduzi kipo hai, kinafuatilia ufanisi wa miongozo, sera na program zake
hivyo kitaendelea kuiagiza serikali itekeleze kila hatua kwa lengo la
kufufua uchumi, kukomesha wizi, ubadhirifu na kutumbua majipu.
Alisema ni jambo la kusikitisha anapowasikia baadhi ya wapinzani wakiwemo
Chadema baada ya kukiri kuwa CCM ni kiboko yao kimeamua kudandia hoja na kusema
ati Dk Magufuli anatekekeza ilani ya upinzani.
"Iko wapi hiyo inayoitwa ilani ya uchaguzi ya upinzani, sikumbuki kama
wana ilani ya uchaguzi. nijuavyo wana shehena ya magunia ya matusi, jeuri na
ubabaishaji si Ilani kama ile ya CCM "alieleza Shaka.
Aidha alisema UVCCM na chama vimempa ruksa na baraka Dk Magufuli azidi
kutumbua majipu, abinye vipele ikiwabhapana budi ayafanyie uoasuaji maeneo yote
yenye uvimbe au uchafu .
Shaka alisema dhamira alionayo Rais Dk Magufuli ni kuhakikisha anarudisha
heshima ya serikali , kuleta mageuzi ya kiutendaji maeneo ya kazi, kupambana na
wahujumu uchumi pia kusadusha kila eneo la utoaji haki na wajibu masuala
hayo yakifanyika .
"Chama chetu hakikufanya kosa kulipitisha jina la Dk Magufuli awe
Mgombea Urais hadi CCM kuifikia uamuzi ule wakubwa wetu waliakini
akiwa mgombea hana makandokando na akipewa nchi atamudu
"alieleza Kaimu huyo Katibu Mkuu .
Msafara wa Mapokezi ya Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka akiwa ziarani Mkoa wa Mara baada ya kuwasili katika Wilaya ya Same
Umati wa wananchi wanachama wa Chama Cha Mapinduzi ukimpokea kwa Shangwe na Nderemo.
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka Akihutubia Umati wa wanachama wa CCM mara baada ya kukabidhi kadi kwa wanachama Wapya
Wanachama wapya wakila kiapo cha chama na Jumuiya katika kikao cha ndani kilicho fanyika katika Wilaya ya Same Magharibi
Wanachama wapya wakila kiapo cha chama na Jumuiya katika kikao cha ndani kilicho fanyika katika Wilaya ya Same Magharibi
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akikabidhi kadi kwa Wanzchama wapya wa Chipukizi mara baada ya kuwasiri katika viwanja vya Stend Kubwa, akiwa katika ziara yake ya Kikazi Mkoani Mara.
Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Ndg. Shaka Hamdu Shaka akimkabidhi kadi ya Chama cha Mapinduzi aliekuwa Mgombea Udiwani Kata ya Kisima Wilaya ya Same kupitia CHADEMA Ndg:Mgonja, baada ya kukihama chama hicho na kujiunga na CCM.
Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg.Shaka Hamdu Shaka akionyesha Kadi mara baada ya kuzipokea wakati wa mkutano wake wa hadhara akiwa katika ziara yake Mkoani Mara.
No comments:
Post a Comment