Habari za Punde

Wizara ya Afya Zanzibar yamuaga KAtibu Mkuu mstaafu Dk Jidawi

 Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na wafanyakazi katika hafla ya kuamuaga Katibu Mkuu aliemaliza muda wake Dkt. Mohd Jidawi (kushoto) na kumkaribisha Katibu Mkuu mpya (kulia) Dkt. Juma Malik Akili alievaa kofia katika Ofisi ya Wizara hiyo Mnazimmoja, Mjini Zanzibar.
 Katibu Mkuu Mstaafu wa Wizara ya Afya Dkt. Mohd Jidawi akiwashukuru wafanyakazi wa Wizara hiyo kwa ushirikiano mkubwa waliompa wakati wa kutekeleza majukumu yake.
 Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo  na Katibu Mkuu mpya wa Wizara hiyo Dkt. Juma Malik Akili wakimsikiliza katibu Mkuu mstaafu Dkt. Mohd Jidawi (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja.
 Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akimkabidhi cheti cha heshima na meza yenye mlango wa Zanzibar (Zanzibar Door), Katibu Mkuu mstaafu wa Wizara hiyo Dkt. Mohd Jidawi katika hafla ya kumuaga iliyofanyika Wizarani, Mnazimmoja. Wa kwanza (kushoto) ni mke wa Dkt. Jidawi, Dkt. Mwanaheri Jidawi.

  Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akimkabidhi mlango wa Zanzibar (Zanzibar Door), Katibu Mkuu mstaafu wa Wizara hiyo Dkt. Mohd Jidawi katika hafla ya kumuaga iliyofanyika Wizarani, Mnazimmoja. Wa kwanza (kushoto) ni mke wa Dkt. Jidawi, Dkt. Mwanaheri Jidawi.
Waziri wa Afya Mhmoud Thabit Kombo, Katibu Mkuu mstaafu na Katibu Mkuu mpya katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi walioshiriki katika hafla hiyo. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.