Habari za Punde

ZSTC Yakabidhi Fidia kwa Wananchi Walioanguja Mkarafuu Wakati wa Uchumaji Zao hilo Kisiwani Pemba.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar, (ZSTC),Ndg.Maalimu Kassim Suleiman, akizungumza na Waathirika walioanguka Mikarafuu katika msimu wa zao hilo kisiwani Pemba kwa mwaka 2015/2016 wakati wa malipo ya fidia, hafla hiyo ya kukabidhi fidia kwa Wabnanchi hao imefanyika katika Ukumbi wa Makonyo Wawi Chakechake Pemba.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Biashara la Taifa (ZSTC), Ndg.Maalimu Kassim Suleiman,akimkabidhi fedha za fidia mmoja ya Mwananchi aliyeaguka Mkarafuu Kiwani Pemba wakati wa hafla ya kukabidi fedha hizo kwa wananchi waliopata ajali za kuanguka mkarafuu kisiwani Pemba hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa makonyo Wawi Chakechake Pemba.Kiwanda cha Mafuta ya Makonyo Wawi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la ZSTC, Maalimu Kassim Suleiman,akizungumza na mtoto ambae alianguka Mkarafuu msimu  wa 2015/2016.huko katika Ukumbi wa Kiwanda cha Mafuta ya Makonyo Wawi.
Mtoto ambae alianguka Mkarafuu msimu uliopita akiweka saini baada ya kukabidhiwa fedha za Fidia kutoka mfuko wa maendeleo ya Karafuu huko Kisiwani Pemba.
Mkurugenzi wa Mfuko wa Maendeleo ya Karafuu Zanzibar, Ndg.Ali Suleiman Mussa, akizungumza na waandishi wa habari kisiwani Pemba kuhusiana na Wananchi waliopata ajali ya kuanguka mkarafuu.(Picha  na Bakar Mussa-Pemba.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.