Habari za Punde

Bawa kubwa la ndege laokotwa kisiwani Pemba

Bawa la Ndege ambayo haijulikani ni ya Nchi gani limeokotwa na Wavuvi wa Kojani Kisiwani Pemba wakati wakiwa katika shughuli zao za uvuvi na kulifikish  ufukweni kwa vyombo husika kwa uchunguzi zaidi. 

Bawa kubwa la ndege limeokotwa na wananchi jana katika Bahari ya Hindi kwenye Kisiwa cha Kojani, Pemba. Haijafahamika ni la ndege ya shirika gani.


Sehemu ambayo inaaminika ni mabaki ya ndege imevuliwa katika bahari ya hindi katika ufukwe wa kisiwa cha kojani pemba.



Bawa la ndege lililopatikana katika bahari ya kisiwa kidogo cha Kojani huko kisiwani Pemba, yamezusha mjadala mkubwa miongoni mwa wakazi wa kisiwa hicho huku wengi wakiamini ni bawa la ndege ya Malaysia ambayo ilipotea bila kujuilikana hatima yake. Ndege ya shirika la Malaysia Airlines yenye chapa MH370, iliotoweka Machi 8 mwaka 2014 haijawahi onekana hadi leo.



Ingawa bado hakuna uhakika ni mabaki ya ndege gani, wataalamu wa usafiri wa anga wamenza hatua ya awali ya uchunguzi wa mabaki hayo ya ndege.



Taarifa zinasema tayari maofisa wa usalama wameanza kulifanyia uchunguzi bawa hilo na huenda si muda mrefu tukapata maelezo ya kutosha kutoka vyombo vinavyohusika

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.