Habari za Punde

Uzinduzi wa Michuano ya Kombe la Mbunge na Mwakilishi Jimbo la Kikwajuni Kati ya Veterani wa Kikwajuni na Vijana G1.Zanzibar Masauni and Jazira Cup.

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na wanamichezo wakati wa uzinduzi wa Kombe la Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni wakati wa mchezo wa Ufunguzi wa michuano hiyo Kati ya Veterani wa Kikwajuni na Vijana wa G1. Masindano hayo yanafanyika usiku katika viwanja vya mnazi mmoja Zanzibar na kushirikisha Timu za Shehia ya Kikwajuu Bondeni,Muembeshauri,Miembeni,Kikwajuni Juu, Kisimanjongoo,Kilimani, na Kilimani Mashariki. 

Mgeni rasmin Waziri wa Afya akiwa katika picha ya pamoja na Timu za hizo wakati wa ufunguzi huo. uliofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja Zanzibar 
Kikosi cha Timu ya G1 kilichokubali kipigo cha bao 2--0 dhidi ya timu ya Veterani wa Kikwajuni wakati wa mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo. 
Kikosi cha Timu ya Veterani wa Kikwajuni wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wao na timu ya G1 uliofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja Zanzibar mabao ya timu ya Veterani yamefungwa na Nonda na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhev Hamad Masauni. kwa shuti la mbali ya eneo la boksi na bao la pili limefungwa na Nonda kwa kupokea krosi iliopigwa na Mhe Masauni.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.