Habari za Punde

Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mh. January Makamba akihutubia wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waliojitokeza katika viwanja vya Mwembeyanga – Temeke katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mbaraka Abdulwakil.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mh. January Makamba akimsikiliza Bw. Charles Leonard Meneja Mradi kutoka Tanzania Forest Conservation Group wakati Mh. Makamba alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho katika viwanja vya Mwembeyanga.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mh. January Makamba akishiriki katika kuzima moto ikiwa ni sehemu ya mafunzo kwa wananchi juu ya namna ya kujihadhari na ajali za moto. Maonyesho hayo yameandaliwa na Jeshi la Zimamoto.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.