Habari za Punde

Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni Wakabidhi Pump ya Maji kwa ajili ya Mradi wa Kisima Jimbo la Kikwajuni Awamu ya Pili kwa Mamlaka ya Maji Zanzibar ZAWA

Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Hamad Yussuf Masauni na Mwakilishi wa Jimbo hilo Mhe Nassor Salum Jazira na Viongozi wa TAYI, wakikabidhi Pump ya Kisima kwa Mradi huo wa kusambaza maji katika Jimbo la Kikwajuni hafla hiyo imefanyika katika Ofisi za TAYI Muembemadema Zanzibar. 
Mbunge wa Jimbo lac Kikwajuni Zanzibar Mhe Hamad Masauni na Mwakilishi wa Jimbo hilo Mhe Nassor Salum Jazira wakikabidhi Vifaa kwa ajili ya Mradi huo wa Kisima kwa Afisa wa ZAWA Ndg. Maulid Hassan. hafla hiyo imefanyika katika Afisi za TAYI muembemadema Zanzibar.  

Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar Mhe. Nassor Salum Jazira akizungumza wakati wa hafla hiyo. 

Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar Mhe Eng. Hamad Masauni akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi Pump ya Kisima kwa Uongozi wa ZAWA ili kukamilisha Mradi kusambaza maji safi na salama kwa jimbo la kikwajuni Zanzibar.
Mwenyekiti wa TAYI Tanzania Othman Abdalla Miraj akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi Pump kwa akili ya Mradi wa Kisima katika Jimbo la Kikwajuni Zanzibar na kuipongeza Mamlaka ya Maji Zanzibar ZAWA kwa ushirikiano wanaotoa katika kufanikisha Mradi huo ukiwa katika Awamu ya Pili kukamilika kwake.
Afisa wa Mamlaka ya Maji Zanzibar ZAWA Ndg Maulid Hassan akitowa shukrani kwa Uongozi wa TAYI kwa ushirikiano wao katika kufanikisha Mradi wa Uchimbaji wa Kisiwa katika Jimbo la Kikwajuni Zanzibar, wakati wa kukabidhiwa Pump ya Kisima kukamilisha Mradi huo awamu ya Pili makabidhiano hayo yamefanyika katika Afisi za TAYI Muembemadema Zanzibar.

1 comment:

  1. Kakabidhi hiyo basi itakuwa shida kweli, huyu jamaa masauni taabu kweli kweli, tushuhudie Matusi sasa siku ikitokea walikosea maji hata kwa dharura ya umeme tu

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.