Habari za Punde

Wananchi wa Uwandani wapigwa marufuku kutumia Ziwa lenye vimelea vya Ugonjwa wa kipindupindu

 VIONGOZI mbali mbali wa Serikali ya Wilaya ya Chake Chake Kisiwani Pemba, wakiangalia moja ya vyoo vinavyotumiwa na wananchi wa shehia ya Uwandani, huku chaoo hicho kikiwa karibu na Ziwa wanalotumia wananchi hao wa Uwandani.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

 VIONGOZI wa Serikali ya Wilaya ya Chake Chake wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe:Salama Mbarouk Khatib akizungumza na mmiliki wa nyumba ambayo choo chake kipo karibu na Ziwa wanalotumia wananchi wa Uwandani.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

 ZIWA ambalo wananchi wa Uwandani wanalitumia kwa ajili ya shuhuli zao mbali mbali, ambalo wamepigwa marufuku kutumia kutokana na kuwepo kwa vimelea vya Ugonjwa wa Kipindu Pindu.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

 MADAKTARI kutoka vitengo vya utabibu katika Wilaya ya Afya Pemba, wakichanganya dawa na maji ya bomba kwa ajili ya kwenda kuyamwaga katika moja ya vyoo vya wananchi wanaoishi karibu na ZIWA la maji ambalo limebainika kuwa na vimelea vya ugonjwa wa kipindupindu huko katika Shehia ya Uwandani.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.