Habari za Punde

Baraza la Manispa Zanzibar Laimarisha Miundombinu ya Maegesho ya Magari Darajani Unguja.

Greda la Baraza la Manispa Zanzibar likitawanya kifusi katika eneo la mchangani Unguja ili kuimarisha miundo mbinu ya maegesho katika Manispa ya Zanzibar ikiwa na upungufu wa maegesho ya magari na kusababisha mshongamano mkubwa na kufikia kuegeshwa magari barabarani na kusababisha foleni kwa watumiaji wa barabara hiyo.

Tayari eneo hili limeimarishwa kwa ajili ya kuegesha magari kwa wananchi wanaofuata mahitaji yao katika maeneo ya mji mkongwe wa Zanzibar likiwa katika hali nzuri baada ya kuimarisha eneo hili la sehemu ya mchangani. Maegesho hayo hutumika kwa magari mbalimbali na kwa ada ya shilingi mia tano.  


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.