Habari za Punde

Baraza la Watoto Zanzibar Latowa Tahadhari kwa Watoto Wenzao Kutukununua Bidha Hatarishi za Kuchezaea Watoto na Kupiga Marufuku Kuuzwa kwa Bidhaa hizo.

                                                                             


Vifaa vya kuchezea Watoto vilivyopingwa marufuku kuuzwa wakati huu wa Sikukuu ya Eid El Fitry kuhusiana na kuwa hatarishi kwa matumizi ya Watoto kusababisha kupofua macho kunakosababidhi vifaa hivyo wanapokuwa wakichezea kwa kutumia bastola bandia kuweka chumbwi hupigana na kuleta athari hizo.
Mratibu wa Mabaraza ya Watoto Zanzibar Unicef  akizungumzia utafiti uliofanywa kuhusiana na matatizo yanayowakuta Watoto wanapofikishwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kitengo cha Macho kesi nyingi ni za kupigwa na Chubwi wakati wa mchezo wao kwa kutumia bastola bandia. 
Mwenyekiti wa Mabaraza ya Watoto Tanzania akitoa Taarifa ya Baraza la Watoto kuhusiana na uuzaji wa bidhaa na Vifaa vya kuchezea Watoto ambavyo ni hatarishi kwa usalama wao wanapokuwa katika michezo yao husababisha kupoteza uono wa macho. Na kueleza takriban Watoto 25 kila mwaka baada ya kumalizika Sikukuu hupoteza macho yao kutokana na Vifaa hivyo hatarishi kwao na kuitaka Taasisi husika kuvipiga marufuku bidha hizo kuuzwa katika viwanja vya Sikukuu na madukani, amevitaja vitu hivyo kuwa Bastola bandia zinazotumia chubwi, baruti, Mishare, Mabovu na venye ncha kali kama mikuki, hupendelea sana Watoto kununua wakati wa sherehe za Sikukuu.  
Mwenyekiti wa Mabaraza ya Watoto Zanzibar akizungumza na waandishi wa habari kulaani uuzaji wa Vifaa hivyo ambavyo ni hatarishi kwa matumizi ya watoto wanapokuwa katika michezo yao.
Daktari wa Kitengo cha Macho hospitali ya Mnazi Mmoja akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kesi za watoto wanazopokea baada ya kumalizika kwa Sikukuu, Watoto wengi hupata athari za macho kwa kupigwa na chubwi au mishare wakati wanapowahoji wanapofika kupatika matibabu ya macho katika hospitali hiyo na kusema takribani kila mwaka hupata kesi kama hizo za watoto 25 na zaidi.  
Daktari wa Kitengo cha Macho hospitali ya Mnazi Mmoja akiwaonesha waandishi wa habari vitu vya kuchezea watoto ikiwemo bastola ya chubwi ambayo huleta madhara kwa mtoto anapopigwa jichoni 
Daktari wa Kitengo cha Macho hopitali ya mnazi mmoja akisisitiza vifaa hivyo vinavyoleta madhara kwa watoto katika macho.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Daktari wa macho katika hospitali ya Mnazi mmoja akitowa maelezo ya athari ya vifaa hivyo vya kuchezea kwa watoto zinazosababisha athari ya macho kwa watoto na hata watu wazima.  

Afisa Biashara katika Wizara ya Biashara na Masoko Zanzibar akizungumza na waandishi wa habari hatua zilizochukuliwa na Wizara yake kuzuiya uingiaji wa bidhaa hizo hatarishi kwa watoto na tayari wizara imeshatowa agizo kwa wafanyabiashara wanaoleta nchini bidhaa hicho kuacha kuleta na kubuni vifaa vigine ambavyo havitakuwa na athari kwa watoto wanapochezea wakiwa katika michezo yao.  Amesema wameandaa timu kupita katika viwanja vya sikukuu kuangalia kama kuna wafanyabiashara wamepuuza agazo hilo na kuwachukulia hatua za kisheria.  
Wajumbe wa Mabaraza ya Watoto wakiwa katika mkutano huo na waandishi wa habari Zanzibar.Waandishi wa habari wakifuatilia maelezo hayo ya Baraza la Watoto Zanzibar wakati wa mkutano huo wa kutoa tamko la kutouzwa kwa bidhaa hatarishi kwa Watoto katika viwanja vya Sikukuu Zanzibar. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.