Habari za Punde

Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa Tanzania Viwanja vya Mnara wa Mashujaa Dodoma leo.

Viongozi wa Kitaifa wakisimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa katika maadhimisho ya siku ya mashujaa yaliyofanyika leo Mjini Dodoma
Askari wa cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakipiga wimbo wa Taifa wakati wa maadhimisho ya siku ya mashujaa yaliyofanyika leo Mjini Dodoma,mgeni rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli,
Vikosi vya ulinzi vikiwa katika Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa katika maadhimisho yaliyofanyika leo Mjini Dodoma ikiwa ni kawaida ya kila ifikapo tarehe kama hii kuwakumbuka  kwa jinsi walivyojitolea kuikomboa nchi yetu
Mchungaji Leonard Muchaicha akiombea dua Mashujaa wakati wa maadhimisho ya siku ya mashujaa yaliyofanyika leo Mjini Dodoma ikiwa ni kawaida ya kila ifikapo tarehe 25/07 kama hii kuwakumbuka  kwa jinsi walivyojitolea kuiko mboa nchi yetu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli pia Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (kushoto) na Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania Generali Devis Mwamunyange wakiwa katika hafla ya maadhimisho ya Mashujaa iliyofanyika leo katika uwanja wa mashujaa Mjini Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli pia Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama alipokuwa akizungumza na  Maelfu ya wananchi wa Mji wa Dodoma leo wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Mashujaa
Baadhi ya maafisa mbali mbali wa Serikali wakiwa katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Mashujaa yaliyofanyika leo katika uwanja wa mashujaa Mjini Dodoma.
Wananchi kwa Maelfu waliweza kuhudhuria katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Mashujaa yaliyofanyika leo katika uwanja wa mashujaa Mjini Dodoma
Wananchi kwa Maelfu waliohudhuria katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Mashujaa wakimshangilia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli pia Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama alipotoa tamko  la Dodoma kuwa makamo Makuu ya Serikali  katika uwanja wa mashujaa Mjini Dodoma leo, [Picha na Ikulu.]

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.