Habari za Punde

PBZ Yaipiga Jeki Hospitali ya Mnazi Mmoja Chupa za Gas ya Oxygen.

Baadhi chpa za Gas ya Oxygen zilizotolewa na Benk ya Watu wa Zanzibar kwa ajili ya matumizi ya Hospitali hiyo ya Mnazi Mmmoja kutowa huduma kwa wagonjwa wanaolazwa katika Hospitali Kuu wakati wakipata hudama, ikiwa ni maadhimisho ya miaka 50 ya PBZ na kusaidia Jamii.  
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ndg Juma Ameir, akisalimiana na Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabi Kombo wakati akiwasili katika hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kukabidhi chupa za Gas ya Oxygen kwa ajili ya matumizi ya hospitali hiyo kutowa huduma kwa wagonjwa wanaopata Tiba. 
Mkurungenzi Mtendaji wa PBZ Ndg Juma Ameir akizungumza wakati wa kukabidhi msaada wa Chupa 150 za Gas ya Oxygen kwa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja, ikiwa ni kuadhimisha miaka 50 ya PBZ na kutoa misaada kwa jamii ndio ilioleta mafanikio ya PBZ kuendelea kwake kutowa huduma kwa Wateja wake karibu Tanzania nzima. 
Mkurungenzi Mtendaji wa PBZ Ndg Juma Ameir akizungumza wakati wa kukabidhi msaada wa Chupa 150 za Gas ya Oxygen kwa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja, ikiwa ni kuadhimisha miaka 50 ya PBZ na kutoa misaada kwa jamii ndio ilioleta mafanikio ya PBZ kuendelea kwake kutowa huduma kwa Wateja wake karibu Tanzania nzima. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ ) Ndg Juma Ameir akikabidhi msaada wa Chupa za Gas ya Oxygen 150 kwa Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Mahmoud Thabit Kombo makabidhiano hayo yamefanyika katika viwanja vya Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja, akishuhudia Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Dk Juma Malik Akili.
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo kulia akipokea msaada wa Chupa za Gas ya Oxygen kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg Juma Ameir Hafidh, kulia kwa Waziri ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Juma Malik Akili. 
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mahmout Thabit Kombo akitowa shukrani kwa Uongozi wa Benki ya Watu wa Zanzibar kwa msaada wao wa Gas ya Oxygen kwa matumizi ya hospitali hiyo.
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akimkabidhi Chupa za Gas ya Oxygen Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Daktari Bingwa Dk Msafiri Marijani.
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Daktari Bingwa Dk Msafiri Marijani akitowa shukrani kwa msaada huo umefika wakati muafaka katika kipindi hichi.umefika wakati ndio ikiwa inahitajika sana. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.