Habari za Punde

Mwanafunzi wa kitanzania ashinda shindano la Insha la Umoja wa Mataifa

 Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Bw. Mogens Lykketoft akiwazungumza washindi 60 wa   Insha kuhusu Lugha Nyingi, Dunia Moja,  miongoni mwa washindi hao  ni mwanafunzi wa Kitanzania Amani Alfred Naburi  anayesoma Chuo  Kikuu cha African Leadership kilichopo  nchini Mauritius wengine katika picha ni Mkuu wa Idara ya Mawasiliano  ya Umma  ya Umoja wa Mataifa,  Bi. Cristina Gallach.

  Amani Alfred Naburi akisoma sehemu ya Insha yake aliyoiandika kwa lugha ya kiingereza ambayo ilizungumzia  lengo namba kumi na moja la maendeleo endelevu ambalo linahusu Miji jumuishi, salama na endelevu. Hafla hii  ilifanyika siku ya Ijumaa katika Ukumbi Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa  Mataifa hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa
 Sehemu ya wanafunzi wa Insha kuhusu Lugha   Nyingi, Dunia Moja wakiwa katika ukumbi Mkuu wa  Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa..Hafla hii ilikuwa ni sehemu ya  Kongamano  la Kimataifa la  Vijana 

Naburi anaonekana  katika mstari wa tatu akishangilia  jambo na wanafunzi wenzie kutoka mataifa mbalimbali duniani ambao  walikusanyika siku ya Ijumaa baada ya kushinda  uandishi wa Insha kwa kutumia lugha sita rasmi zinazotumika katika Mikutano ya Umoja wa Mataifa.

Na   Mwandishi Maalum, New   York

Mwanafunzi wa  Kitanzania, Amani Alfred Naburi,   ni mmoja wa  kati ya  wanafunzi 60 kutoka     Vyuo  Vikuu mbalimbali  duniani ambao wameshinda shindano la  Insha   ijulikanayo kama   “Lugha nyingi, Dunia Moja” ( Many  languages, One World) lililoandaliwa kwa ushirikiano baina ya  United Nations Academic Impact ( UNAI) na ELS Educational Services, Inc.

Jumla ya  wanafunzi  3,600 kutoka mataifa 165 walijitokeza kuwania  shindano  hilo   ambalo hatimaye  majaji waliwaibua wanafunzi  60 kutoka mataifa 36  kama washindi wa  shindano hilo.

Amani Alfred Naburi ni  mtanzania  anayesoma   Chuo Kikuu cha  African Leadership University,  huko Mauritius. Baadhi ya  masharti ya  kuingia shindano  hilo  lilitaka mshiriki  lazima awe ni  mwanafunzi aliye

Washindi hao 60  walipata fursa ya kusoma sehemu ya  Insha yao  mbele ya  washindi wenzao  na  washiriki  wengine waliokuwa wakihudhuria kongamano  la  vijana, katika hafla iliyofanyika kwenye  ukumbi Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hapa Makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Mbali ya washindi hao  60 kuzungumza, wazungumzaji  wakuu  wengine  walikuwa ni   ambayo  Rais wa Baraza Kuu Bw. Mogens Lykketoft na  Bi Cristina Galach Naibu Katibu Mkuu  Msaidizi Mwandamizi anayesimamia idara ya  Mawasiliano ya Umma ya Umoja wa Mataifa na   Mjumbe Maalum wa  Katibu Mkuu  kuhusi  Vijana  Bw. Ahmad Alhendawi  aliwasilisha  Salamu za Katibu Mkuu  Ban Ki Moon.

Washindani wa Insha hiyo  walitakiwa kuandisha Insha  juu ya namna watakavyochangia katika utekelezaji  wa  Malengo  Mapya ya Maendeleo Endelevu ( Agenda (2030). Ambapo  kila moja wapo alitakiwa kuiandika insha  hiyo   yenye  maneno yasiyozidi 2,000 kwa  lugha  nje ya lugha yake ya   asili ya nchi anayotoka.

Tafsri yake ni kuwa  walitakiwa kuandika   kwa  lugha sita ambazo ni rasmi na zinazotambuliwa    na kutumika na Umoja wa Mataifa. Lugha hizo ni  Kiingereza, Kifaransa,  Kiarabu, Kichina, Kispanishi na  Kirusi

Malengo  waliyopewa washindani hao   kuyandikia maoni hayo ni   lengo namba kumi na mbili  linalozungumzia Matumizi na  Uzalishaji Bora (  Ensure Sustainable consumption and production ) lililowasilishwa kwa lugha ya   Kifaransa,   lengo namba   kumi na sita  ambalo linazungumzia  kuhusu Amani,  Haki na Taasisi Imara ( Promote just, peaceful and inclusive societies) lilowasilishwa kwa  Kirusi,  lengo  namba kumi na tano  linaluhusu Uhai juu ya Ardhi( Sustainably manage  forests, combat desertification, halt and reverse land degradation, halt biodiversity loss ) lilowasilishwa kwa Kispanishi

Malengo mengine ni  lengo  namba kumi na tatu  kuhusu  kuchukua  hatua kwa  mbadiliko ya Tabia nchi  na  athari zake ( Take urgent action to combat climate change and its impacts), lengo namba tisa kuhusu  Viwanda,  Ubunifu na  Miundo Mbinu (  Build resilient infrastructure, promote sustainable industrialization and foster innovation), lengo  namba kumi na moja    kuhusu kuifanya  miji kuwa jumuishi,  salama,  na endelevu  ( make cities Inclusive, safe, resilient and  sustainable). Lengo hilo ndilo ambalo  
Mwanafunzi  Amani   Naburi  aliliandika insha kwa lugha ya kiingereza kiasi cha kukoga nyonyo za  majaj.

Lengo kuu la uandishi wa  insha  kwa lugha sita  rasmi zinazotumika katika umoja wa Mataifa ni pamona na mambo mengine, kuwawezesha wanafunzi kujifunza lugha na tamaduni za  nchi nyingine ,  kupanua wigo na fursa ya kujifunza mambo na changamoto zinazoikabili dunia na kujaribu kutoa mawazo yao  yatakayoweza kusaidia katika kuzikabili changamoto hizo.

Lengo   jingine ni kuwawezesha  wanafunzi kutambua uwezo na vipaji vyao  kama  njia  moja wapo ya kuwaandaa kuwa   viongozi wa taifa la kesho.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.