Habari za Punde

Onesho la Filamu ya Mchezo wa Mpira wa Miguu wa Wanawake Zanzibar.

Msaidizi Kocha wa Timu ya Taifa ya Wanawake Tanzania Nassra Juma akitowa maelezo ya filamu yao inayoonesha michezo ya mpira wa miguu wa timu za Zanzibar wakati wa Jukwaa la Filamu la Nchi za Jahazi Zanzibar ZIFF lililofanyika katika viwanja vya Ngome Kongwe Zanzibar. Liloazi kurindima kuazia tarehe 7 July na 17, lilipotua tanga lake usiku wa jana baada ya kumaliza maonesho yake mbalimbali.  Wachezaji wa Timu ya Wanawake wakifuatlilia filamu ya Kabumbu Zanzibar ikioneshwa katika Jukwaa la Filamu la ZIFF, wakati wa maonesho yake ya filamu mbalimbali zilizopasi katika Tamasha hilo la 19 la Nchi za Jahazi Zanzibar lililomalizika jana katika viwanja vya ngome kongwe Zanzibar   
Wageni wakiwa katika viwanja vya ukumbi wa Ngome Kongwe Zanzibar wakifuatilia maonesho ya filamu zilizooneshwa wakati wa Tamasha hilo la ZIFF, wakiangalia filamu ya mchezo wa mpira wa wanawake wa timu za Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.