Habari za Punde

Sala ya Eid El Fitr viwanja vya Maisara na mkono wa Eid Ikulu

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akijumuikana Viongozi mbali mbali na Waislamu wengine katika swala ya Sunna ya Eid el Fitri ambayo huswaliwa baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, iliyoswaliwa leo katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 06/07/2016.
  Waumini wa Dini ya kiislamu wakiwa katika swala ya Sunna ya Eid el Fitri iliyoswaliwa leo katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan,ambapo Viongozi mbali mbali walijumuika,[Picha na Ikulu.] 06/07/2016
baadhi ta aBaadhi ya wananchi kadhaa waliofika katika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja katika  kusherehekea Sikukuu ya Eid el Fitri baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan wakisubiri kupewa mkono wa Eid na Rais Dk Ali Mohamed Shein,[Picha na Ikulu.] 06/07/2016.


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akizungumza na Mashekhe waliofika Ikulu Mjini Unguja kupeana mkono wa Sikukuu na kutakiana kheri ikiwa ni kusherehekea Sikukuu ya Eid el Fitri baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan,[Picha na Ikulu.] 06/07/2016.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimkabidhi bahasha Mzee Suleiman Khamis wa Darajabovu (kulia) alipokuwa akitoa sikukuu kwa wananchi mbali mbali waliofika katika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja katika  kusherehekea Sikukuu ya Eid el Fitri baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan,[Picha na Ikulu.] 06/07/2016.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.