MATANGAZO MADOGO MADOGO

Monday, July 18, 2016

Shirika la Bandari Lapata Crane Mpya Mbili kwa Ajili ya Kutowa Huduma Bandani ya Unguja na Moja Bandari ya Pemba.

Shirika la Bandari Zanzibar lapata Crane mbili kubwa na ndogo kwa ajili ya kutowa huduma ya upakizi na ushushaji wa mizigo katika bandari yac Unguja na Pemba, kutoka kampuni ya Ujerumani iliotengeneza Crane hiyo. Crane kubwa ina uwezo wa kubeba mzigo wa tano 64 kwa wakati mmoja kushsha katika meli na kupakia katika meli kama inavyoonekana Crane hiyo ikishusha katika meli bandari ya Zanzibar.  
Crane kubwa ya Shirika la Bandari ikiwa katika bandari hiyo baada ya kushushwa, Crane hiyo itapunguza tatizo la ushushaji wa mizigo katika meli wakati meli hizo zikiwa na matatizo ya crane katika meli hiyo. 
Mtaalamu wa Kampuni ya Ujerumani iliotengeneza Crane hiyo akitumia remote ya kuongozea Crane hiyo wakati ikiwa katika bandari ya Zanzibar.

Crane Ndogo ya Shirika la Bandari ikishushwa katika Meli hiyo ambayo itatumika katika Bandari ya Mkoani kisiwanin Pemba.