Habari za Punde

Urafiki wa Tanzania, China ugeukie kumaliza dawa za kulevya


Ulianzia kabla ya Tanganyika na Zanzibar kuungana mwaka 1964

Na Haji Nassor, Pemba

DUNIA inalia, Afrika inalia na Tanzania inalia kutokana na wimbi la biashara ya dawa za kulevya.

Kila mmoja anaelewa fika athari zilizomo kwenye utumiajia wa dawa hizo haraumu hasa kwa vijana wetu.

Sio tu kwamba eti zina athari kiafanya, lakini hata kukosa vija madubuti ambao ndio wapiga kura, madaktari, mabalozi, mawaziri, na watendaji wa kuu wa taifa letu hapo baadae na sasa.

Hivi sasa duniani kuna watu zaidi ya milioni 15.9 kutoka nchi 151, wanaojidunga dawa za kulevya aina mbalimbali kama vile kokeni, heroine, amphetamines na nyingine kama hizo, ambazo ni hatari.

Ukisikia takiwmu za dunia, jua kuwa hata Tanzania imo humo, jambo ambalo sio jema hata kidogo, na iweje tusivume kwa mambo mema kama ya soka, mkakusanyo ya ushuru na bandari za kisasa.

Na kwamba watu milioni 3 kati ya hao wanaojidunga dawa za kulevya wamepata maambuziki ya virusi vya Ukimwi na kwamba kasi ya maambukizi ya virusi hivyo ni kubwa kwa watu wanaojidunga sindano za dawa hizo.

Shirika la Kimataifa la Medecins du Monde (MdM), ambalo linashughulika na kutoa misaada mbalimbali ya kibinadamu ya hasa kwenye nchi na maeneo yaliyoathiriwa na magonjwa,
vita, majanga ya asili, njaa na umasikini, lipo pia Tanzania ambapo husaidia jamii kwenye nyanja mbalimbali.


Mradi huo uko kwenye nyanja tofauti, kama vile kutoa elimu kwa walengwa kuhusu madhara na hatari ya matumizi ya dawa hizo, kutoa ushauri na upimaji wa virusi vya Ukimwi, kuzuia na kutibu maambukizi ya magonjwa ya ngono.


Miaka ya 1980 dawa aina ya heroini na kokeni za rangi ya kahawia zilianza utumika nchini na baadhi ya watu, kisha mwaka 1990, ndipo matumizi ya dawa za kulevya kwa njia ya kujidunga ikaanza.

Hata hivyo mapema mwaka 2000 dawa za kulevya aina ya heroine nyeupe, ikaanza kuingia nchini na watumiaji wakaendelea kuongezeka hata hivyo, taarifa kuhusu watumiaji wa dawa hizo ilipatikana kuwa watu takribani 200,000 nchini wanatumia dawa hizo.


Taarifa ambazo sio rasmi kuhusu idadi ya watumiaji wa dawa hizo hivi sasa nchini, imeongezeka hadi kufika watu kati ya 200,000 hadi 250,000 ndio wanatumia dawa za kulevya.


Aidha kati ya watumiaji hao, watu 25,000 wanatumia dawa za kulevya kwa njia ya kujidunga sindano za heroine na kati ya hao 18,000 ni wakazi wa jiji la Dar es Salaam, pekee.

Tanzania watumiaji wengi wa dawa za kulevya hutumia
heroine kwa kuwa ni rahisi na hata upatikanaji wake na hutumika kwa njia ya kujidunga sindano.


Tanzania na China inaurafiki wa muda mrefu katika sketa mbali mbali kama za kihabari, afya, michezo na kisiasa, sasa wakati umefika kwa taifa la Tanzania, ambalo nalo linazongwa na dawa za kuelevya kukopi na kupesti inavyofanya China.

Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka juzi, idadi ya vifo vinavyotokana na matumizi ya dawa za kulevya ilifikia 49,000 na hasara za kichumi za moja kwa moja zinazotokana na matumizi ya dawa za kulevya kila mwaka zimefikia ya bilioni 500.

Naamini upo urafiki wa kweli baina ya Tanzania na China, sasa tuwashawishi, tuwabembeleze, tuwaombe ili watupe mbinu na njia sahihi za kupambana na dawa za kulevya nchini.

Inawezekana kwenye mahakama zetu, sheria zetu hapo ndio penye tatizo, sasa wakati umefika kwa Tanzania kutokana na ufariki wake na China, kuangalia namna walau ya kupunguza wimbi la uingiaji na matumizi ya dawa za kulevya.

Kwa mfano kulikua na kesi 18 mwaka juzi za dawa za kulevya zilizokuwa zikisikilizwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, zimefutwa kwa sababu zilisajiliwa kimakosa katika katika mahakama hiyo na washtakiwa wanapandishwa upya kizimbani.

Mkuu wa Kitengo cha Kuzuia Dawa za Kulevya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Godfrey Nzowa wakati huo, alipoulizwa kuhusu kufutwa mfululizo kwa kesi hizo, alisema kesi hizo zinazofutwa zipo katika orodha ya kesi zilizopo Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam kwa ajili ya kusikilizwa.

Sasa hapa utanona jinsi ya kesi za dawa za kulevya nchini Tanzania ambapo kama zinakwenda zigi zaga, ambapo kwa rafiki wetu mkubwa wa nchi hii, yaani China mambo ni tofauti.

“Zipo kesi nyingi na zitaendelea kufutwa kutokana na Mahakama Kuu kufanya makosa kuzisajili katika kitabu cha kesi za uhujumu uchumi,” alisema.

Mwaka 2013 Jeshi la Polisi Tanzania lilisema, kuwa wanawake wawili raia wa Tanzania, walitambuliwa kuwa ndiyo wanaodaiwa kuingiza shehena ya dawa za kulevya zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 6.8 nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania.

Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na dawa za Kulevya, Geofrey Nzoa, alisema haijafahamika wanawake hao wanatoka mikoa gani hapa nchini.

Wanawake hao walikamatwa na maofisa wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini, wakiwa na masanduku sita ambayo yalipokaguliwa yalikutwa na takribani kilo 150 za dawa hizo, ambazo pia zinajulikana kama ‘Tik’ zikiwa na thamani ya bei ya mtaani ya Randi milioni 42 sawa na shilingi bilioni 6.8.

Alisema kumekuwa na wimbi kubwa la Watanzania wanaojiingiza katika biashara haramu ya dawa za kulevya, ndani na nje ya nchi na kwamba, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, watuhumiwa 10,799 walikamatwa kwa kujihusisha na dawa hizo.


Lazima Tanzania ikope mikoba ya kama ya ufundi kutoka nchini China, ili alau Tanzania itishe kwa kuona dawa za kulevya ni kosa la jinai lisilopaswa kufanyiwa mzaha.

Wapo wengi wanaosema kuwa, kukamatwa na dawa za kulevya nchini China, haichukui muda kifo humnyemelea mtuhumiwa, au hata kifungo cha kuoezea jela, jambo ambalo imekuwa mfano wa kuingwa na kuogopewa na mataifa mengine. 

Taarifa za mitandao zinaoneyesha kuwa, watanzania wamekuwa sugu kukoma biashara ya dawa za kulevya, maana mwaka juzi, watanzania 240 walikamatwa katika nchi za Brazil, Pakistan na Afrika Kusini, na hivyo kuharibu taswira ya nchi yetu.


Kama kuna jambo ambalo linaichafuaTanzania katika jukwaa la kimataifa kwa siku hizi, basi ni tatizo la usafirishaji wa dawa za kulevya.


Zamani tatizo hili halikuwa kubwa sana, ni mtanzania mmoja mmoja sana alikuwa akikamatwa nje, kwa kusafirisha dawa za kulevya.

Kwa hiyo jina la nchi yetu lilikuwa linasikika mara moja moja, au kwa bahati mbaya kuhusiana na tatizo la dawa za kulevya.
Lakini katika siku za hivi karibuni tumesikia kuwa kuna watanzania wanakamatwa Ulaya, Amerika Kaskazini, Amerika 
Kusini, Asia na hata katika nchi za Afrika.

Mitandao inatuhabarisha kuwa China, mpaka sasa naweza kusema kwa sasa tatizo limefikia kiwango cha kutia hofu, na hasa kwa mji wa Hong Kong na ambako kuna wafungwa zaidi ya 100 wa kitanzania.

Tofauti na siku za nyuma, ambapo sasa idadi ya wafungwa wa kike inazidi kuongezeka, ambapo kwa sasa kuna wafungwa wa kike zaidi ya 20 katika magereza ya China na Hong Kong.

Hapa nadhani kwa viongozi wetu wasikivu wa Tanzania, wakageuza shilingi upande wa pili, ili urafiki uliopo baina yetu na China sasa umalize dawa za kulevya.

Hivi karibuni tumesikia alichokifanya Dk Mwakyembe kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere, yeye anaona kuwa uwanja unaobeba jina la Mwalimu Nyerere haupaswi kuhusishwa na dawa za kulevya.

Alichofanya Dk Mwakyembe pale uwanjani hapo, kwa kweli ni jambo zuri, na kama asingefanya hivyo huenda watanzania tungeendelea kuwa kizani kuhusiana na mambo yanayoweza kuwa yanaendelea katika forodha zetu.

Aliekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Mhe. Fatma Abdulhabib Fereji amesema dawa za kulevya ni janga la kidunia linalopigwa vita na Mataifa yote duniani

Iweje urafiki wa China na Tanzania ambao ulianza hata kabla ya mwaka 1964, tusiwashawishi walau kutupa mbinu, fikrasa, mawazo za kupunguza kama sio kumaliza dawa za kulevya.

Zanzibar inakadiriwa kuwa na watumiaji wa dawa za kulevya zaidi ya 9,000 idadi ambayo ni kubwa, kwa mujibu wa idadi yote ya waakazi milioni 1.3,(2012), jambo ambalo linahatarisha maisha ya vijana kujiingiza zaidi katika utumiaji huo.

Uhusiano baina ya China na Tanzania umeleta maendeleo ya muda mrefu na yenye kasi, tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia baina ya mataifa hayo mawili.
Kwa mujibu wa mitandao China ilianzisha uhusiano wa kidiplomasia na Tanganyika Desemba 9, 1961 na Zanzibar Desemba 11, 1963.

Wakati Tanganyika na Zanzibar zilipoungana na kuwa Tanzania Aprili 26, 1964, ilikuwa ni suala la moja kwa moja kwa China kuendeleza uhusiano wake wa kidiplomasia na Tanzania. 

Taarifa ya tovuti ya wizara ya mambo ya nje ya China inaonyesha kuwa mwaka 2007, biashara kati ya Tanzania na China ilifikia thamani ya dola milioni 290, ambapo kati ya hizo bidhaa za China, nchini zilifikia thamani ya dola milioni 180 wakati iliagiza kutoka Tanzania bidhaa za thamani ya dola milioni 110. 
 

Kama haya mazuri, yapo sasa wakati ndio huu kwa China kuigeukia Tanzania kupiga vita dawa za kulevya, ambazo zinaendelea kuiathiri Tanzania ambayo ni rafiki wa miaka mingi.
Tena hasa kwa sasa rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania wa awamu ya tano, John Pombe Magufuli, ambae kabla na baada ya kuingia Ikulu ya Tanzania, alishawaahidi watanzania kuwa atapambana na dawa za kulevya.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.