Habari za Punde

Chuo cha ZIBRET Kikiwa Katika Matayarishi ya Kupata Usajili wa Kutoa Shahada ya Kwanza.

Mkuu wa Taaluma wa Chuo cha Zibter Ndg Khatib Mjaka  Hamad akizungumza na Waandishi wa habari wa Vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar akitowa Taarifa ya Chuo hicho kikiwa katika harakati za kupata Usajili wa kutoa Shahada ya Kwanza (Bachelor Degree ) katika mwaka wa masomo wa 2017/2018, Na kusema kwa sasa Taasisi hiyo imepata ithibati ya kuendesha Kozi kubwa nne Kutoka Baraza la Taifa la Elimu ya Juu ya Ufundi (NACTE) kwa ngazi ya Cheti na Stashahada ya (Diploma) ambazo hutolewa na Chuo hicho ni. Islamic Banking and Finance, Information and Communication Technilogy. Business Administration na Procurement and Supply. 

Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali Vilioko Zanzibar wakifuatilia Taarifa ya Chuo cha ZIBRET kuanza kutoa Shahada ya Kwanza kwa mwaka wa masoma 2017/2018. mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Chuo hicho Mwanakwerekwe Zanzibar.
 Waandishi wakifuatilia mkutano huo. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.