Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)akisalimiana na Bw,Mauricio Ramos,Mtendaji Mkuu wa kampuni ya "Millicom Group"akiwa na ujumbe wake walipofika Ikulu Mjini Unguja kwa mazungumzo leo (kushoto) Nd,Benoit Janin Mtendaji Mkuu wa Zanztel ,[Pivha na Ikulu.]23/08/2016.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Bw,Mauricio Ramos,Mtendaji Mkuu wa kampuni ya "Millicom Group"akiwa na ujumbe wake walipofika Ikulu Mjini Unguja kwa mazungumzo leo,[Pivha na Ikulu.]23/08/2016.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Bibi Rachel Samren Naibu Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Millicom Group pia Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Zanztel (katikati) Bw,Mauricio Ramos,Mtendaji Mkuu wa kampuni ya "Millicom Group"(wa pili kulia) na (kushoto) Nd,Benoit Janin Mtendaji Mkuu wa Zanztel ujumbe huo ulifika Ikulu Mjini Unguja leo kwa mazungumzo na Rais,[Pivha na Ikulu.]23/08/2016.
STATE
HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF
THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 23.08.2016
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.
Ali Mohamed Shein ameeleza haja kwa Kampuni ya simu ya ZANTEL kupitia Kampuni ya “Millicom Group”
kuimarisha utoaji huduma zake ili kuweza kupata mafanikio zaidi katika
ushindani wa kibiashara.
Dk. Shein aliyasema
hayo katika mazungumzo kati yake na uongozi wa Kampuni ya ZANTEL ukiongozwa na
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya “Millicom Group” akiwa pamoja na Naibu Mtendaji
Mkuu wa Kampuni ya “Millicom Group” na Mwenyekiti wa Bodi ya ZANTEL Rachel
Samren pamoja na Mtendaji Mkuu wa ZANTEL Benot Janin.
Katika mazungumzo hayo
Dk. Shein aliueleza uongozi huo kuwa kufanikiwa kwa Kampuni hiyo ya simu ya
ZANTEL katika utoaji huduma zake ndani na nje ya nchi ndio njia moja wapo ya
kuitangaza Zanzibar kimawasiliano sambamba na kuinua uchumi wa Zanzibar.
Dk. Shein alisema kuwa
kutokana na kuwepo kwa Kampuni nyingi za simu ambazo zimekuwa zikitoa huduma
kwa wananchi Kampuni hiyo ya ZANTEL ina kila sababu ya kuimarisha huduma zake
ili iendelee kuwa kivutio KWa wananchi katika kupata huduma bora za mawasiliano
ya aina zote hapa nchini.
Aidha, Dk. Shein
alitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa Kampuni hiyo ya ZANTEL kwa kuendelea kuwa
na makao makuu yake hapa Zanzibar.
Pamoja na hayo, Dk.
Shein aliueleza uongozi huo kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendeleza
ushirikiano wake na Kampuni hiyo ambayo Serikali ina hisa zake kwa lengo la
kutoa huduma bora za mawasiliano kwa wananchi.
Pamoja na hayo, Dk.
Shein aliitaka Kampuni ya Millicom iendelee kujikita katika kuiwezesha ZANTEL
kukuza na kuimarisha ukuaji na upanuzi wa shughuli zake hapa nchini.
Kwa upande wa Mkonga
wa Taifa, Dk. Shein aliueleza uongozi huo haja ya kufuata taratibu zilizowekwa
ili kila upande upate mafanikio pamoja na matarajio waliyojiwekea katika
kuimarisha mawasiliano hapa nchini.
Nae Mtendaji Mkuu wa
Kampuni ya “Millicom Group” Mauricio Ramos, alimueleza Dk. Shein kuwa Kampuni
hiyo itahakikisha ZANTEL inapata mafanikio zaidi kutokana na mikakati madhubuti
iliyowekwa.
Alieleza kuwa juhudi
mbali mbali zinaendelea kuchukuliwa katika kuhakikisha ZANTEL inaendelea
kupanua soko lake sambamba na kuimarisha miundombinu yake ili kuweza kutoa
huduma za uhakika.
Mtendaji Mkuu huyo wa Kampuni ya “Millicom Group” alimueleza Dk. Shein kuwa
ZANTEL itahakikisha inakuwa mstari wa mbele katika kuimarisha huduma zake ikiwa
ni pamoja na kupanua mtandao unaotumia 4G ambayo inarahisisha mawasiliano.
Sambamba na hayo, uongozi huo ulipongeza mashirikiano mazuri inayoyapata
kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambayo ina asilimia 15 za hiza za
ZANTEL na kuahidi kwa upande wao kuendelea kuzidisha ushirikiano huo kwa lengo
la kutoa huduma kwa jamii sambamba na kuimarisha uchumi wa Zanzibar.
Kampuni ya Millicom
ilitangaza kuanza utekelezaji wa mpango wa uwekezaji katika Kampuni ya ZANTEL
ambao unajumuisha uimarishaji wa huduma za mtandao wa Kampuni hiyo ambapo Kampuni
ua “Millicom Group” ilinunua asilimia 85 ya hisa za ZANTEL.
Rajab
Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax:
024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment