Habari za Punde

Waziri Gavu Azungumza na Waandishi kwa Kukamilika kwa Maandalizi ya Mkutano wa Kongamano la Tatu la Diaspora Zanzibar.

 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Issa Haji Gavu akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar kuhusiana na kukamilika kwa maandalizi ya Kongamano la Mkutano wa Diaspora unaotarajiwa kufanyika Zanzibar kesho katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort na kuhudhuriwa na Wanzanzibar na Watanzania wanaoishi Nje na kuhudhuriwa na karibu Madiaspora 346  wanaotegemewa kushiriki kongamano hilo.
Waziri Gavu akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo akijibu majibu ya waandishi wa habari kuhusiana na mkutano huo. 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Issa Haji Ussi Gavu akionesha moja ya waraka wa kuimarisha Diaspora Zanzibar kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Jumba la Forodhani. 
Waandishi wakiwa katika mkutano huo wakimsikiliza Waziri Issa akitowa maelezo kwa waandishi wa habari. No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.