Habari za Punde

Mbunge na Mwakilishi wa jimbo la Tunguu Zanzibar, Khalifa Salim Suleiman na Simai Mohamed Said wamekabidhi vifaa vya michezo (jezi na mipira) kwa vilabu vya Wadi ya Ubago na Wadi ya Tunguu vyenye thamani ya sh.milioni 10.

 Mbunge wa jimbo la Kwahani Zanzibar, Dk.Hussein Mwinyi (mwalikwa) akisalimia wanamichezo wa Wadi ya Tunguu jimbo la Tunguu Zanzibar akiambatana na Mwakilishi wa jimbo  la Tunguu, Simai Mohamed Said (kushoto) wakati wa kukabidhi vifaa vya michezo vilivyotolewa na Mbunge na Mwakilishi wa Tunguu jana.


 Mwakilishi wa jimbo hilo, Simai Mohamed Said akizungumza na wanamichezo wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa iliyofanyika kwenye Wadi ya Tunguu.
Mtunza hazina wa klabu ya  Woman Fighters ya Jumbi, Mariamu Haji (kulia) akipokea vifaa kutoka kwa Mbunge Khalifa Salim Suleiman (kati) na Mwakilishi Simai Mohamed Said (kulia) Kushoto ni Mbunge wa viti maalumu wanawake mkoa wa Kusini Unguja, Mwatum Dau.
Picha na Martin Kabemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.