Habari za Punde

Wajumbe wa bodi ya mfuko wa barabara watembelea barabara ya Bahanasa-Mtambwe

 NAIBU katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar, Shomar Omar Shomar akiwafahamisha jambo wajumbe wa Mfuko wa Barabara Zanzibar, wakati walipokagua matengenezo yanayoendelea kufanywa na kampuni ya MECCO katika barabara ya Bahanasa-Mtambwe, barabara zilijengwa na Kampuni ya H-YOUNG.(Picha Na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 NAIBU katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar, Shomar Omar Shomar akimfahamisha kitu msimamizi wa matengenezo yanayoendelea kufanywa katika barabara ya Bahanasa-Mtwambe na Kampuni ya MECCO Injinia Ombeni Olegenes, wakati wajumbe wa bodi ya mfuko wa barabara walipotembelea barabara hiyo.(Picha Na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 WAJUMBE wa Bodi ya Mfuko wa Barabara Zanzibar, wakiangalia moja ya matengenezo yanayoendelea kufanywa katika barabara ya Bahanasa-Mtambwe na kampuni ya MECCO, wakati wa ziara yao ya kutembelea barabara mbali mbali za Kisiwa Cha Pemba.(Picha Na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 WACHIMBAJI wa Msingi wa kuwekea bomba la Maji, uliopo karibu na barabara wakiendelea na kazi yao licha ya kipindi cha nyumwa kusimamishwa kutokuchimba msingi huo, kwa kuwa upokaribu na barabra ya Konde-msuka, hatiame wajumbe wa bodi ya Mfuko wa barabara Zanzibar umesimamisha kazi hiyo isiendelea hadi Wizara mbili Miundombinu Mawasiniano na Usafirishaji na Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira zitakapokutana.(Picha Na Abdi Suleiman, PEMBA.)
INJINIA Mkaazi wa Wizara ya Miundombinu Mawasiliano na Usafirishaji Khamis Massoud Mwenyeshati la mikono mirefu, akitoa maelezeo kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Shomar Omar Shomar, wakati wakiangalia kazi ya Uchimbaji wa Msingi wa kuwekea bomba la Maji katika barabra ya Konde-Msuka, msingi huo ulio karibu na barabra hiyo.(Picha Na Abdi Suleiman, PEMBA.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.