Habari za Punde

Waathirika walioanguka kutoka kwenye mikarafuu walipwa fidia

 Mkurugenzi wa Mfuko wa Maendeleo ya Karafuu Zanzibar, Ali Suleiman, akizungumza na Waathirika walioanguka kutoka kwenye mikarafuu katika msimu huu wa 2015/2016 , huko katika ukumbi wa kiwanda cha mafuta ya makonyo Wawi kabla ya kufanyika malipo ya fidia.
 Mkurugenzi Muendeshaji wa Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) Dk, Said Seif Mzee, akizungumza na Wananchi na waathirika walioanguka kutoka kwenye mikarafuu katika msimu huu wa mwaka 2015/2016 huko katika kiwanda cha mafuta ya makonyo Wawi.


.

Baadhi ya Waathirika walioanguka mikarafuu msimu huu wa 2015/2016 wakiwemo na watoto wakimsikiliza Mkurugenzi muendeshaji wa ZSTC, huko katika ukumbi wa Kiwanda cha Mafuta ya Makonyo Wawi .

 Mkurugenzi wa Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) Dk Said Seif Mzee, aakikabidhi fedha za fidia ya Wananchi walioanguka mikarafuu msimu huu wa 2015/16 huko katika ukumbi wa Kiwanda cha makonyo Wawi Pemba.
Ofisa Mdhamini shirika la ZSTC Pemba, Abdalla Ali Ussi, akizungumza na Waathirika walioanguka mikarafuu msimu huu wa 2015/2016 huko katika ukumbi wa Kiwanda cha Mafuta ya Makonyo Wawi.


 Mkurugenzi wa Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) Dk Said Seif Mzee, aakikabidhi fedha za fidia ya Wananchi walioanguka mikarafuu msimu huu wa 2015/16 huko katika ukumbi wa Kiwanda cha makonyo Wawi Pemba.

Picha ya pamoja kati ya Waathirika walioanguka Mikarafuu msimu wa 2015/16 na Uongozi wa Shirika la biashara la Taifa Zanzibar  (ZSTC) Zanzibar, huko nje ya ukumbi wa Kiwanda cha Mafuta ya Makonyo Wawi-Pemba.Picha na Bakar Mussa -Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.