WAZEE walioathirika wa Ungonjwa wa Ukoma wanaoishi
Makundeni Kinyasini Wilaya ya Wete, wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Wizara
ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Zanzibar, Mhe:Maudline
Cyrus Castico, wakati alipowatembelea wazee hao huko wanakoishi na kuwajuulia
hali.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MMOJA wa wazee walioathirika na ugonjwa wa Ukoma
Makundeni Kinyasini Hamadi Abdalla, akitoa maelezo juu ya historia ya wazee hao
na kuwepo hapo Makundeni kwa waziri wa Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee,
Vijana, Wanawake na Watoto Zanzibar, Mhe:Maudline Cyrus Castico, wakati
alipowatembelea wazee hao.(Picha na Abdi
Suleiman, PEMBA.)
WAZIRI wa Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana,
Wanawake na Watoto Zanzibar, Mhe:Maudline Cyrus Castico, akimsikiliza kwa
makini mmoja wa wazee wanaoishi katika nyumba ya wazee Gombani Chake Chake
Pemba, wakati alipowatembelea wazee hao katika ziara yake ya siku mbili
Kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman,
PEMBA.)
WAZIRI wa Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana,
Wanawake na Watoto Zanzibar, Mhe:Maudline Cyrus Castico, akikabidhi baskeli za
walemavu kwa wazee wanaoishi katika nyumba ya wazee Gombani Chake Chake Pemba,
ikiwa ni msaada kutoka kwa Makamo wa pili wa rais wa Zanzibar Mhe:Balozi Seif
Ali Iddi, kulia ni mtunzaji wa wazee wa Limbani Wete Jadi Mohamed Jadi.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MMOJA wa Wazee wanaoishi katika nyumba ya wazee
Gombani akimueleza jambo, Waziri wa Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana,
Wanawake na Watoto Zanzibar, Mhe:Maudline Cyrus Castico, wakati alipowatembelea
wazee hao katika nyumba yao.(Picha na
Abdi Suleiman, PEMBA.)
WAZIRI wa Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana,
Wanawake na Watoto Zanzibar, Mhe:Maudline Cyrus Castico,akiwa katika picha ya
pamoja na wazee wanaolelewa katika nyumba ya wazee Gombani Chake Chake Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
No comments:
Post a Comment