Habari za Punde

Jamii yatakiwa kupiga vita ndoa za umri mdogo

Mwashungi Tahir  Na Khadija Khamis                        Maelezo



 Jamii inatakiwa kuwa mstari wa mbele kupiga vita ndoa  katika umri mdogo kutokana na athari ambazo zinazoweza kujitokeza na kuhatarisha maisha ya mama na mtoto.

Hayo yameelezwa na Mwanasheria wa Zafela Salma  Suleiman huko katika  jengo la malaria Mwanakwerekwe  kwenye semina  ya kupinga ndoa  za utotoni na udhalilishaji wa wanawake na watoto  iliyowashirikisha wazazi, walimu wa vya madrasa pamoja na masheha.

Amesema jamii ipewe elimu zaidi ili ndoa hizo zisiweze kuendelea ambazo zinaweza kuhatarisha maisha ya watoto pamoja na kuzidisha umaskini katika jamii.

Aidha watoto chini ya umri wa miaka 18 viungo vyao vinakuwa bado havijakomaa kwa kuweza kujifungua kwa njia salama hivyo kunauwezekano mkubwa wa kupata  matatizo wakati wa kujifungua .

Alieleza jamii ielewe faida na hasara za ndoa hizo kwani kupelekea ongezeko la watoto  wa mitaani , pamoja na maradhi ya zinaa ambayo hupelekea kupata maradhi ya maambukizi .

Pia alielezea kuwa serikali  imetunga sheria ya elimu, na sheria za makosa  ya  jinai  ya mwaka 1984 ambayo imetoa adhabu  kwa mtu yeyote ambae atamfanyia  mtoto suala la udhalilishaji  chini ya umri huo.

“Sheria ya elimu  inamfanya  mtoto atakapo  pata uja uzito baada ya kujifungua ndani ya miaka miwili kwa wakati wowote  anaruhusika kurudi kuendelea na masomo yake , “Alisema Salma .

Vile vile kwa mzazi au mlezi ambae atachukua  hatua ya kumuozesha mtoto mwenye umri mdogo ataingia hatiani kwa mujibu wa sheria ya kosa la jinai na kutozwa faini kwa mujibu wa makosa ,kisheria.

Sambamba na hayo mwanasheria huyo alisema kesi za udhalilishaji zinaongezeka siku hadi siku kutokana na uzorotaji wa kutolewa hukumu  kwa kesi hizo na kuongezeka kwa  malimbikizo ya kesi hizo.
Akitoa msisitizo kwa wazazi na walezi kuepuka adhabu za kuwanyima vyakula , kumpiga kupita kiasi kunaweza kukampelekea uzururaji wa mitaani  na kupata udhalilishaji wa kubakwa

Nae sheha wa shehia ya Mpendae Haji Seti  ameitaka jamii isivunjike moyo wakati inapotokea kesi ya ushalilishaji kwenda mahakamani kwa kila siku hadi itapotolewa hukumu ya kesi hiyo

 “Wazazi pamoja na mashahidi huvunjika moyo  kwa muda mwingi unaotumika kwa kutolewa hukumu  kwani daktari tayari amekwisha thibitisha ushahidi wake lakini tatizo ni kwa waendeshaji mashtaka wanataka ushahidi usio na shaka jambo  ambalo halitowezekana.”walisema baadhi ya wazee hao .

Amewataka wazazi wawe mstari wa mbele kwa kufatilia kesi hizo pindipo zinapotokea hadi pale mahakama inapofikia hatua ya kutoa  maamuzi yaliyo sahihi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.