Mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu Afisi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Ndg Amour Mohammed akizungumza wakati wa mkutano huo. uliofanyika katika Afisi za Baraza kutoa taarifa ya kukamilika kwa Mkutano wa Baraza la Wawakilishi.
Mkuu wa Shughuli za Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mussa Kombo akifafanua jambo wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari Zanzibar.
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar wakimsikiliza Mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu wa Afisi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Ndg Amour Mohammed akizungumza kuhusiana na kukamilika kwa matayarisho ya Mkutano wa Baraza unaotarajiwa kuaza 21,Septemba2016.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA
YA SHUGHULI ZA MKUTANO WA TATU WA BARAZA
LA TISA LA WAWAKILISHI
UTAKAOANZA TAREHE 21 SEPTEMBA, 2016
Mkutano wa Tatu wa Baraza la
Tisa la Wawakilishi Zanzibar unatarajiwa
kuanza siku ya Jumatano tarehe 21 Septemba, 2016, saa 3:00 asubuhi.
SHUGHULI
ZITAKAZOFANYIKA.
Shughuli za Mkutano huo
zitakuwa kama ifuatavyo:-
1.
Maswali
na Majibu.
Maswali 184
yatajibiwa kwenye Mkutano huu.
2.
Miswada
ya Sheria
Miswada ya Sheria
iliyowasilishwa na kusomwa kwa mara ya Kwanza katika Mkutano wa mwezi Mei, 2016
itasomwa kwa mara ya pili na tatu na kujadiliwa katika Mkutano huu wa
Tatu.
Miswada yenyewe ni:-
i)
Mswada
wa Sheria ya Kurekebisha Sheria ya Chuo Kikuu cha Zanzibar, Nam. 8 ya 1999 Kama
ilivyorekebishwa na Sheria Nam. 11 ya 2009 na Kuweka Masharti Bora Pamoja na
Mambo Mengine Yanayohusiana na
Hayo.
ii)
Mswada wa Sheria ya Kuanzisha Taasisi ya Elimu ya
Zanzibar na Mambo mengine
Yanayohusiana na Hayo.
iii)
Mswada wa Sheria ya Usimamizi (Utafutaji na Uchimbaji) wa
Mafuta na Gesi Asilia, Kuanzisha Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Utafutaji
na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia, Kuanzisha Kampuni ya Maendeleo ya Mafuta
na Kuhakikisha Uwajibikaji wa Taasisi za Mafuta na Mambo Mengine Yanayohusiana
na Hayo.
iv)
Mswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbali Mbali na
Kuweka Masharti yaliyo Bora kuhusiana na
Mambo Hayo.
v)
Mswada wa Sheria ya Marekebisho ya
Katiba ya Zanzibar ya 1984.
vi)
Miswada minne (4)
kusomwa kwa mara ya kwanza
3. Marekebisho ya Kanuni za Baraza la
Wawakilishi Toleo la 2012.
(Amour M. Amour)
Kny. Katibu
Baraza
la Wawakilishi, Zanzibar
Tarehe 19 Septemba,
2016
No comments:
Post a Comment