Habari za Punde

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said Azuru Kaburu la Baba Yake Marehemu Mohammed Said na Makaburi ya Familia Yao katika Kisiwa cha Uzi Wilaya ya Kati Unguja.

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said, akiwa na Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe Maudline Castico, wakielekea katika makaburi ya Ukoo wa Mhe Simai wakati akiwa katika ziatra ya Kisiwa cha Uzi kuzindua Mabaraza la Vijana wa Shehia ya Uzi kulia kwa Mwakilishi Mzee wa Uzi Omar Khamis Ali.   
Mhe. Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto Mhe Maudline Castico na Mhe Mwakilishi wa Jimbo la Uzi Simai Mohammed Said wakiitikia dua ikisomwa na Mzee wa Uzi Omar Khamis Ali, walipofika kuzuru makaburi hayo ya Vizazi vya Mhe Simai. kulia ni kaburi la Marehemu Mohammed Said, aliyezikwa huko katika kisiwa cha Uzi Wilaya ya Kati Unguja. 
Mzee wa Kisiwa cha Uzi Omar Khamis Ali akisoma duas kuwaombea Wazazi wa familia ya Mhe Simai, walikozikwa Wazazi wa Baba yake Marehemu Mohammed Said, Bibi yake Mwanakweli Simai Hassan na Babu wa Baba yake Mzee Simai Hassan, wamezikwa katika makaburi hayo huko katika Kijiji cha kwa Kisiwa cha Uzi Wilaya ya Kati Unguja.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe, Simai Mohammed Said akimuonesha Mhe Waziri Maudline Castico kaburi la Babu wa Baba yake Mhe Simai Mohammed Said , anayeitwa Simai Hassan wakati walipofika kutembelea makaburi haro na kuomba dua kwa marehemu, ikiwa katika ziara yake katika kisiwa cha Uzi kuzindua Mabaraza ya Vijana ya Shehia ya Uzi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.