Habari za Punde

Oman yaonesha nia ya kulikarabati jengo maarufu la Beit al Ajaib (House of Wonders)


Jengo  maarufu  la  Beit  Al Jaib (  House of Wonders) ambalo   Serikali ya Tanzania inaiomba Serikali ya Oman kuangalia  uwezekano wa kulikarabati   kama sehemu ya mradi wa kuhifadhi nyaraka, kumbukumbu na majengoa ya kihistoria  visiwani  Zanzibar

 Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na  Sultanate of Oman,  Dkt Augustine Mahiga ( kushoto) na  Yusuf bin Alawi bin Abdullah wakizungumzia kuhusu namna ya kuendelea kuimarisha uhusiano  mzuri baina ya  nchi hizo mbili.  Katika  mazungumzo hayo Waziri Mahiga ameiomba  serikali ya Oman kupitia  Waziri Abdullah kuangalia uwezekano wa  kushirikiana katika  uhifadhi ya  nyaraka na kumbukumbu  muhimu  pamoja na  ukarabati ya  jengo la  House of Wonders lilojengwa na ufalma wa Oman  mwaka  1883
Waziri wa  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa  Afrika Mshariki, Augustine Mahiga akizungumza na  Naibu Waziri wa  Mambo ya Nje wa Marekani  anayehusika na  masuala ya Afrika,  Mazungumzo yao yalijielekeza zaidi katika uhusiano na ushirikiano  kati ya  nchi hizi mbili

Na Mwandishi Maalum, New  York

Ufalme wa Oman umeonesha nia ya  kukarabati  majengo  ya makubusho ya kale   ya  Beit Al Jaib  maarufu kama “ House  of  Wonders” yaliyopo  mjini  Unguja – Zanzibar.

Nia hiyo imeoneshwa na   Waziri wa Mambo ya   Nje wa  Oman,  Bw. Yusuf bin Alawi bin Addullah wakati   alipokutana na kufanya  mazugumzo na  Waziri wa Mambo ya Nje  na  Ushirikiano wa  Afrika Mashariki, Dkt, Augustine Mahiga.

Mazungumzo  baina ya  viongozi  hao wawili  yalifanyika  pembezoni mwa  Mkutano wa 71 wa  Baraza Kuu la  Umoja wa Mataifa, ambapo  Mawaziri hao walikuwa wakiongoza ujumbe wa Nchi  zao.

Mazungumzo   ya   Mawaziri  hao  yalijikita  katika   uimarishwaji wa uhusiano  na ushirikiano mzuri  uliopo  baina ya  Oman na  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 Katika majadiliano hayo ambapo   pamoja  na  mambo mengine,  Waziri  Mahiga  aliomba  serikali ya Oman kuangalia uwezekano  wa kuanzishwa  kwa miradi wa kutunza mambo ya kale zikiwamo nyaraka muhimu zinazohusu uhusiano  baina ya nchi  hizo mbili

Waziri Mahiga  alieelezea  pia hali uchakavu wa  majengo ya   Beit Al Jaib ( House of wonders)   majengo yaliyokuwa  Ikulu ya  utawala wa Kifalme, Zanzibar.  Makubusho hayo  yamesheheni historia ya  uhusiano  na ushirikiano kati  ya  Zanzibar na   Sultanate of Oman na  Afrika  Mashariki kwa Ujumla.

Na kutokana na historia hiyo na  umuhimu wa  jengo hilo ambalo limejengwa mwaka 1883, Waziri ameiomba  Serikali ya  Oman kuangalia  uwezekano wa kulihifadhi jingo hilo ambalo pia ni kivutio kikubwa cha utalii.

Akijibu  ombi  hilo na  mengine yaliyowasilishwa na   Waziri Mahinga,  Waziria wa Mambo ya Nje wa Oman,  Bw .   Yusuf bin Alawi bin Addullah amemtaka  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa  Afrika   Mashariki kuandaa andiko  na  kuliwasilisha  katika Serikali ya  Oman ili  pendekezo  hilo liweze  kufanyiwa kazi pamoja na mapendekezo mengine.

Katika  hatua nyingine,  Waziri wa Mambo ya Nje  na  Ushirikiano wa   Afrika Mashariki,  Augustine  Mahiga amekuwa na   kuwa  na mazungumgo na   Bi. Linda Thomas Greenfield,   Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayehusika na  masuala ya   Afrika.

Mazungumzo ya  Waziri Mahinga na   Bi.  Linda Greenfield yalijikita zaidi  katika uhusiano na  ushirikiano  baina ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Marekani.



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.