STATE
HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF
THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 27.09.2016
RAIS wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amemtumia salamu za
pongezi Rais wa Jamhuri ya Watu wa China
Xi Jinping kwa kutimiza miaka 67
tokea kuundwa kwa Taifa hilo.
Dk. Shein, alieleza kuwa kwa niaba yake binafsi pamoja na wananchi
wote wa Zanzibar wanatoa pongezi kwa Rais Xi, wananchi wa China pamoja na
Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kwa kutimiza umri huo wa Taifa hilo tokea
kuasisiwa kwake.
Salamu hizo zilieleza kuwa Watu wa Zanzibar
wanapata faraja na matumaini kutokana na maendeleo makubwa yanayoendelea kupatikana
katika Taifa hilo la China kwenye sekta mbali
mbali za maendeleo na uchumi.
Aidha, salamu hizo zilieleza kuwa Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na wananchi wake wataendelea kutoa ushirikiano sambamba
na kuimarisha uhusiano mkubwa uliopo kati yao na ndugu zao wa China.
Pamoja na hayo, salamu hizo za pongezi
zilimtakia afya njema na mafanikio ya muda mrefu Rais wa Jamhuri ya Watu wa
China Xi Jimping katika kuliongoza Taifa hilo.
Rajab Mkasaba, Ikulu
Zanzibar
Postal Address:
2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment