Habari za Punde

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ziarani Kisiwani Pemba Atembelea Kaburi la Dk Omar Ali Juma Wawi.

Wapiganaji wa JWTZ wakiwa na maua maalumu kwa ajili ya kumkabidhi rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe: John Pombe Magufuli na mke wake mama Janet Magufuli, ili kuyaweka juu ya kaburi la aliekuwa makamu wa rais Dk Omar Ali Juma alifariki mwaka 2001,
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe: John Pombe Magufuli, akipokea shada la maua kutoka kwa mpiganaji wa JWTZ Pemba,  kwa ajili ya kuliweka kwenye kaburi la aliekuwa Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk, Omar Ali Juma kijijini kwoa Wawi Chakechake Pemba
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe: John Pombe Magufuli, akiweka shada la maua juu ya kaburi la aliekuwa Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dk, Omar Ali Juma, kijijini kwao Wawi Chakechake Pemba
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe: John Pombe Magufuli, mama Janet Magufuli, akipokea shada la ma ua kutoka kwa mpiganaji wa JWTZ, kwa ajili ya kuliweka kwenye kaburi la aliekuwa Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dk, Omar Ali Juma aliefariki mwaka 2001 na kuzikwa kijijini kwao Wawi Chakechake Pemba
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe: John Pombe Magufuli, mama Janet Magufuli, akiweka shada la maua juu ya kaburi la aliekuwa Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dk, Omar Ali Juma kijijini kwao Wawi Chakechake Pemba
Sheikh. Rashid Abdalla akiomba dua kwa pamoja, kwenye kaburi la aliekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk: Omar Ali Juma, wakati rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk: John Pombe Magufuli na ujumbe wake walipolizuru kaburi lake, liliopo Wawi Chakechake, Pemba
Baadhi ya wananchi wa shehia ya Wawi wilaya ya Chakechake Pemba, wakiwa wamenyanyua mikono juu, kumuombea dua aliekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk: Omar Ali Juma wakati rais wa Jamhuri ya Muungano wa Dk: John Pombe Magufli alipokwenda kulizuru kaburi hilo
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe: John Pombe Magufuli, akisaini kitabu cha wageni, muda mfupi baada ya kufika kwenye kaburi la aliekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Omar Ali Juma kijijini kwao Wawi wilaya ya Chakechake Pemba, kabla ya kulizuru kaburi lake, 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe: John Pombe Magufuli, akizungumza na wananchi wa shehia ya Wawi wilaya ya Chakechake Pemba, muda mfupi baada ya kulizuru kaburi la aliekuwa Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk, Omar Ali Juma kijijini kwao Wawi Chakechake Pemba.

 (Picha na Haji Nassor, Pemba).


  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.