Mahujaji wa kutoka Tanzania wapatao 2,000
waliwasili salama katika miji mitakatifu ya Makkah na Madina mwishoni mwa mwezi
Agosti mwaka huu na tayari wameshaanza kufanya ibada pamoja na ziara hadi
katikati ya mwezi Septemba mwaka huu.
Hakuna taarifa zozote za matatizo kuhusu mahujaji
wa Tanzania katika maeneo waliyofikia, wote wako salama na afya njema.
Mwaka huu Serikali ya Saudi Arabia imeimarisha
miundo mbinu, usafiri, ulinzi, usalama na uangalizi makini kuhakikisha kuwa
hakuna dosari zozote zinazoweza kutokea kutokana na uwepo wa wingi wa mahujaji
kutoka nchi mbalimbali duniani. Takriban mahujaji milioni 2 kutoka mabara yote
duniani wapo nchini Saudi Arabia kutekeleza nguzo mojawapo kati ya nguzo 5 za
dini ya kiislamu.
Taarifa imetolewa na:
Balozi Hemedi Iddi Mgaza
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia
B
Balozi
wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Iddi Mgaza wa Pili kutoka kulia
akipata chakula cha pamoja na viongozi wa vikundi mbalimbali vya mahujaji
kutoka Tanzania katika mojawapo ya makazi ya mahujaji mjini Makkah. Wa tatu
kutoka kulia ni Rais wa vikundi vyote vya Mahujaji BIITHA Sheikh Abdallah
Talib, wa kwanza kushoto ni Rais wa taasisi za Hijja kutoka Zanzibar UTAHIZA
Sheikh Ali Adam na wa kwanza kulia ni Mkuu wa Utawala Ubalozini Bw. Ahmada
Sufiani Ali.
Viongozi
na mahujaji wakiendelea kupata chakula cha pamoja.
No comments:
Post a Comment