AFISA wa
Mamlaka ya Maji (ZAWA) Wilaya ya Micheweni Ali Rajab Khatib, akitoa maelezo ya
mradi wa maji uliojengwa na TASAF II katika shehia ya Wingwi Njuguni, kwa
wajumbe wa kamati ya Baraza la Wawakilishi ya Kusimamia Ofisi za Viongozi wakuu
Kitaifa, wakati walipotembelea miradi mbali mbali iliyo chini ya Ofisi ya
Makamo wa Pili wa Rais Ofisi ya Pemba.(Picha
na Abdi Suleiman, PEMBA.)
WAJUMBE wa Kamati ya Baraza la Wawakilishi ya
Kusimamia Ofisi za Viongozi wakuu wa Kitaifa, wakipata maelekezo ya mashine ya
maji iliyotolewa na kuwekwa nyengine ambayo kwa sasa haikidhi mahitaji ya
wananchi katika kisima hicho, kilicho jengwa na mradi wa TASAF II katika shehia
ya Wingwi Njugumi Wilaya ya Micheweni Pemba.(Picha
na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MWENYEKITI wa Kamati ya Baraza la wawakilishi ya
kusimamia Ofisi za Viongozi wakuu wa kitaifa, Mwakilishi wa jimbo la Konde
Mhe:Omar Said Abeid, akizungumza afisa wa Mamlaka ya Maji ZAWA Wilaya ya
Michweni Ali Rajab Khatib, wakati kamati yake ilipotembelea mradi huo wa maji
huko Wingwi Njuguni.(Picha na Abdi
Suleiman, PEMBA.)
MJUMBE wa Kamati ya Baraza la Wawakilishi ya
Kusimamia Ofisi za Viongozi wakuu wa Kitaifa, Mwakilishi wa Jimbo la Mpendae,
Mhe:Mohamed Said Dimwa, akieleza jambo wakati wajumbe wa kamati hiyo
walipokagua mradi wa maji safi na salama Wingwi Njuguni.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MJUMBE wa kamati ya Baraza la Wawakilishi ya
kusimamia Ofisi za Viongozi wa kuu wa Kitaifa, Mwakilishi wa jimbo la Tunguu
Mhe:Simai Mohamned Simai (Mpaka Basi), akitoa mawazo juu ya mradi wa maji safi
salama Wingwi Njuguni uweze kufikia malengo.(Picha
na Abdi Suleiman, PEMBA.)
AFISA mdhamini Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais
Pemba, Mhe:Ali Salum Mata, akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa kamati wa baraza la
wawakilishi, juu ya Mradi wa Maji safi na salama Wingwi Junguni.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
WAJUMBE wa kamati ya baraza la Wawakilishi ya
Kusimamia Ofisi za Viongozi wa kuu wa Kitaifa, Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu
Mhe:Simai Mohamed Simai na Mwakilishi wa Jimbo la Mpendae Mhe:Mohamed Said
Dimwa wakisokota kamba kwa kutumia mashine maalumu, huku wajumbe wenzao
wakiwaangalia juu ya ufanyaji wa kazi hiyo.(Picha
na Abdi Suleiman, PEMBA.)
NDEGE kubwa aina ya Precision Air, ikiwa inashusha
mizigo baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Karume Air Port Kisiwani Pemba,
kama inavyoonekana katika Picha .(Picha
na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MWAKILISHI wa Jimbo la Mpendae Mhe:Mohamed Said
Dimwa, akiwauliza maswali wafanyakazi waliopo katika mashine ya kuchunguzia
Mizigo katika Uwanja wa Ndege wa Pemba.(Picha
na Abdi Suleiman, PEMBA.)
WAJUMBE wa kamati ya Baraza la Wawakilishi ya
kusamamia ofisi za Viongozi wa kuu wa Kitaifa, wakiwa katika kikao cha pamoja
cha Tathmini ya ziara yao, kilichofanyika Ofisi ya Makamu wa Pili Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais
Zanzibar Mhe:Mohamed Aboud Mohamed, akizungumza wajumbe wa kamati ya baraza la
wawakilishi ya kusimamia Ofisi ya Viongozi wa kuu wa Kitaifa, huko katika
ukumbi wa Tasaf Pemba.(Picha na Abdi
Suleiman, PEMBA.)
No comments:
Post a Comment