Habari za Punde

Hotuba ya Shukurani iliyotolewa na Mmiliki wa kampuni ya Pennyroyal katika semina ya BLW


Hotuba ya Shukrani Iliyotolewa na Bwana.Brian Thomson –Mmiliki na Mkurugenzi wa Kampuni ya Pennyroyal (GIBRALTAR) Limited Zanzibar.
Katika Semina na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika Ukumbi wa Hoteli ya Ocean View - Chuini Zanzibar. 24 ktoba 2016


 Mheshimiwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Mheshimiwa Spika wa Baraza la Wawakilishi, na Mwenyekiti wa 

Mkutano Huu Muhimu.

Mheshimiwa Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi.

Waheshimiwa Mawaziri na Manaibu Mawaziri;

Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu;

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini, Unguja 

Mheshimiwa Mwenyekiti wa CCM Kaskazini, Unguja.

Wwaheshimiwa Sana Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ;

Washiriki Kutoka Taasisi za Serikali;

Waandishi wa Habari;

Mabibi na Mabwana;

Itifaki Imezingatiwa,


Mheshimiwa Mwenyekiti,

Mabibi na Mabwana,

Ni heshima kubwa kwangu kupata fursa hii adhimu ya kutakiwa 

kutoa neno la shukrani katika semina hii muhimu na ya kihistoria.  

Kwa niaba ya Kampuni ya Pennyroyal (Gibraltar) Limited, 

wafanyakazi wote, washiriki waliokusanyika katika ghafla hii na 

kwa niaba yangu binafsi, napenda kutoa shukrani za dhati kwako 

kwa kutumia muda wako adhimu na kuwa na sisi leo kwa ajili ya 

kubadilishana mawazo na kutupa moyo wa kuendelea kutekeleza 

azma yetu, tukiamini kuungwa mkono na wewe na Waheshimiwa 

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Mabibi na Mabwana,

Sisi, (Pennyroyal), tunamtambua na tunatoa shukrani kwake 

Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein – Rais wa Zanzibar na 
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kutuunga mkono, 
kutupa ushauri, kutupa moyo na kutuongoza - jambo ambalo linatupa uhakika wa kufanikisha utekelezaji wa Mradi wa Amber Resort.  Dira na hamu ya Mheshimiwa Rais ni kuiona Zanzibar kupitia mradi huu inapiga hatua kubwa na ya kipekee itakayoifanya Zanzibar kuwa kivutio kikubwa cha dunia cha utalii, lakini inayotambulika kimataifa na yenye kukabili ushindani.


Mabibi na Mabwana,

Tuko hapa leo kuonesha azma na malengo yetu kwa Serikali na 

kwa Wazanzibari, kupitia nyinyi Waheshimiwa sana Wajumbe wa 

Baraza la Wawakilishi, ambao mnawawakilisha jamii yote ya 

Zanzibar kutoka kila eneo la visiwa hivi, kwamba Mradi wa 

Amber Resort utachangia sana ukuaji wa uchumi wa Zanzibar na mabidiliko yake, lakini pia utachangia kubadilisha na kuleta maisha bora kwa jamii ya wengi.  Kwa mnasaba huo na kwa umuhimu mkubwa mulionao, tunawaomba Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kusikiliza kwa makini mawasilisho yetu, baadae mutoe maoni na fikra zenu na muulize maswali, lakini mwisho wa siku, nyinyi kama wadau wetu, tunakuombeni muwe Mabalozi wa Pennyroyal kwa umma wa Zanzibar, kutoa uelewa na kuunga mkono azma hii ili iweze kufanikiwa utekelezaji wake kwa manufaa ya Visiwa hivi.

Mheshimiwa Mwenyekiti,

Mabibi na Mabwana,

Kabla ya kumaliza hotuba hii fupi, niruhusu nichukue fursa hii 

adhimu kuitambulisha timu ya Pennyroyal niliyokuja nayo leo hii, 

ambayo imekuwa ikifanya kazi kubwa sana kwa mradi huu, na 

kuhakikisha inatimiza ndoto na hamu yetu hapa Zanzibar.  Leo 

nimekuja na timu na, naomba niwataje kama ifuatavyo:-

1.    TIA EGGLESTONE
2.    MOHAMMED ISSA KHATIB
3.     GASPER NYIKA
4.     BOBBY MCKENNA
5.     SALEH MOHAMED SAID

Mwisho, lakini si kwa umuhimu wake, naomba kutambua ushiriki 

na kazi kubwa iliyofanywa na Mheshimiwa Spika na Ofisi yake, 

kwa maandalizi mazuri yaliyofanikisha shughuli yetu hii.  Kwa 

niaba ya Pennyroyal na timu nzima na kwa niaba yangu binafsi, 

napenda kuchukua fursa hii kuweka katika kumbukumbu shukrani 

za dhati kwako Mheshimiwa Spika na Ofisi yako kwa kuunga 

mkono juhudi zetu.  Tunawashukuru sana.


Ahsanteni nyote kwa kunisikiliza.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.