Habari za Punde

ITC ya Mchezaji wa Zanzibar Babi Yawasili Visiwani

Na Mwandishi Wetu. 

Baada ya kushindwa kumtumia kwenye michezo yake minne iliyopita kiungo mshambuliaji wao Abdi Kassim Sadallah maarufu Babi au Ballack wa Unguja, mashabiki wa Taifa ya Jang'ombe wameanza kucheka.



Furaha hiyo inakuja kufuatia Shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA, kuwasilisha kibali cha mchezaji huyo - ITC kwa Chama cha Mpira wa miguu Zanzibar.


Kibali hicho kilichoombwa mapema mwezi huu kilichelewa kuwasilishwa na kupelekea mchezaji huyo kushindwa kuonekana uwanjani wakati timu yake ilipokua inapambana.


Kupatikana kwa kibali hicho cha Kimataifa kumewafanya mashabiki wa timu hiyo kushusha presha kwani wanaimani kubwa kuwepo kwa Babi uwanjani kutaisaidia timu yao kulamba alama tatu kwa wapinzani wao.



Abdi Kassim alilazimika kutafutiwa kibali hicho kutoa FIFA kutokana na kumalizia msimu wake wa ligi nchini Malaysia akiwa na klabu ya UiTM.



Bila shaka mashabiki wa Taifa na wapenda soka wa Zanzibar wataanza kumuona mchezaji huyo kesho saa moja usiku wakati timu yake itakapochuana na klabu ya Mafunzo ikiwa ni mwendelezo wa ligi kuu ya soka Zanzibar. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.