Habari za Punde

Semina ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Kuhusiana na Mradi wa Kijiji cha Utalii Matemwe (Penny Royal ) Zanzibar.


Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid akisalimiana na Muwekezaji wa Mradi wa Hoteli ya Kitalii ya PennyRoyal Bwana Brian Thomson, awakati akiwasili katika ukumbi wa mkutano wa Semira ya kutowa maelezo ya Utekelezaji wa Mradi huo kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean Kihinani Zanzibar.
Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Mgeni akizungumza wakati wa Semina hiyo na kumkaribisha Mgeni Rasmin Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zuberi Ali Maulid kufungua Semina hiyo ya Siku Moja kuzungumzia changamoto za Mradi huo. wa Kijiji cha Utalii Matemwe Zanzibar. 
Baadhi ya washiriki wa Semina hiyo wakiwa katika ukumbi wa Mkutano katika hoteli ya Kitalii ya Zanzibar Ocean Kihinani Zanzibar.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid akizungumza wakati wa mkutano wa Semina ya Siku moja kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuhusiana na Mradi wa Ujenzi wa Kijiji cha Utalii Matemwe PennyRoyal. Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa hoteli ya kitalii ya Zanzibar Ocean Kihinani Zanzibar Wilaya ya Magharibi B Unguja.   
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid akifungua Semina hiyo ya Siku Moja kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar. 
Maofisa wa ZIPA wakifuatilia Semina hiyo wakati wa ufunguzi uliofanywa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid. kuzungumzia utekelezaji wa Mradi huo Mkubwa kwa Nchi za Afrika Mashariki.  
Wawakilishi wa Kampuni ya Penny Royal ya Ujenzi Mradi wa Kijiji Utalii Matemwe wakimsikiliza Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zuberi Ali Maulid akifungua Semina hiyo kwa Wajumbe wa Baraza katika Ukumbi wa Hoteli ya Kitalii Zanzibar Ocean Kihinani Zanzibar.  
Mwenyeviti wa Wenyeviti wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Hamza Hassan akizungumza wakati wa Semina hiyo na kutowa maelezo kabla ya kuwasilishwa mada za ujenzi wa mradi huo na swahusika kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Viongozi wa meza kuu wakimsikiliza Mwenywviti wa Wenyeviti wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Hamza Hassan wakati akizungukmza katika semina hiyo baada ya kufunguliwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kuzungumzia faida kwa Zanzibar baada ya kukamuilika kwake mradi huo jinsi Wananchi wa Zanzibar watakapofaidia kupitia Mradi huo katika nyanja mbalimbali katika jamii ya Zanzibar.






























Waziri wa Ardhi Maji Nishati na Mazingira Zanzibar Mhe Salama Aboud Talib akijibu haja za michango ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakati wa Semina ya Wajumbe kuhusiana na Mradi wa Ujenzi wa Kijiji cha Utali Matemwe Zanzibar, Changamoto unaoukabili Mradi huo, Semina hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Z-Ocean Kihinani Wilaya ya Magharibi B Unguja. Na kuhudhuriwa na Wadau mbalimbali wa Sekta za Serikali Zanzibar. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.