Habari za Punde

Kamati Mpya ya Rufaa ZFA Yakabidhi Zana Zake.

Katibu mkuu wa Chama cha mpira wa miguu Zanzibar Kassim Haji Salum leo ameikabidhi rasmi vitendea kazi kamati mpya ya Rufaa na Usuluhishi ya Chama hicho.

Akikabidhi zana hizo huko uwanja wa Amaan, Kasaim alisema kamati hiyo ni miongoni mwa kamati tano ambazo zimeundwa kwa lengo la kupunguza mzigo kwa kamati tendaji ya ZFA hiyo.

Kiongozi huyo alidai kuwa kwa sasa zfa inaendelea kuboresha suala zima la usimamizi wa soka kwa kushirikisha wajumbe tofauti na wale waliozoeleka kwenye kamati tendaji.
Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya kamati yake, katibu mteule Suleiman Haji maarufu Kibabu aliahidi kufanya kazi kwa mujibu wa katiba na kanuni ya Chama hicho na kuondokana na mazoea.

Kikabu alisema kamwe hakutokua na suala la muhali katika kusimamia kanuni na kamati yake itakua ikitoa maamuzi pasipo kuangaliana usoni.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.