Rais wa Kampuni ya Rafiki Network Bwana Hamad Omar Hamad |
Na: A.O. Ali
Kampuni mashuhuri ya filamu ya Banyak
kutoka nchini Uingereza, imetangaza nia na dhamira yake ya kufanya kazi pamoja
na kampuni ya Rafiki Network nchini
Tanzania katika kufanikisha tukio lake la kwanza la resi ndefu za ngalawa
litakalofanyika tarehe 18 Disemba, 2016, huko Vumawimbi kisiwani Pemba visiwani
Zanzibar.
Akitoa taarifa
huyo kwa mwandishi wa habari hii kupitia mazungumzo ya simu, Rais wa kampuni ya
Rafiki Network Bwana Hamad Omar Hamad amethibitisha kuwa mazungumzo kati yao na
kampuni ya Banyak yameshakamilika na kwa sasa kampuni hiyo inakamilisha utaratibu
wa kujiandaa kwa ajili ya tukio hilo.
“ Napenda
niwahakikishie kuwa baada ya kuliona wazo letu hili la kutaka kuanzisha
resi ndefu za ngalawa hapa Afrika
Mashariki, wenzetu wa BANYAK wa kule Uingereza hawakufikiri mara mbili.
Wamesema wako tayari kuja nchini kushirikiana nasi kikamilifu.” Alisema Bwana Hamad.
Aidha Bwana
Hamad amesema amefarijika sana kuwa licha ya kuwasiliana na wadau wengi wa
biashara yakiwamo mashirika ya simu, ndege na usafiri wa baharini, imempa moyo
sana kuona kwamba kampuni hii ya kigeni ndiyo imekuwa ya kwanza kuona fursa
adhimu na kujitokeza kushiriki katika tukio hili adhimu na la kihistoria
nchini.
“ Wenzetu wa
Banyak hawakujali tukio hili linaandaliwa na nani, wapi na vipi. Baada ya kuona
baadhi ya maandiko na posta ya tangazo la
tukio letu, imewatosha wao kuona kuwa kuna fursa kubwa katika tukio hili. Kwa
kutambua umhimu wa tukio lenyewe wameamua kuchukua gharama na muda wao kuja
kushiriki kikamilifu katika kufanikisha tukio letu hili. Kwa kweli ni habari
njema sana kwetu!” Alisema Bwana Hamad.
Kampuni ya
Banyak ni moja kati ya kampuni mashuhuri nchini Uingereza ambayo kwa muda mrefu
imekuwa ikijishughulisha na kuandaa makala za video (documentary) zenye
kuelimisha jamii. Kampuni hiyo yenye
makazi yake jijini London, itaingia makubaliano ya kurikodi tukio zima la resi
za ngalawa zitakazofanika Pemba mwishoni mwa mwaka huu. Resi hizo ndefu zaidi
kuwahi kutokea katika pwani ya Afrika Mashariki zitaanzia bandari ya Vuma wimbi
na kuishia bandari ya Tumbe, takribani mwendo wa kilomita 30 za baharini.
Resi hizo
zitashirikisha Ngalawa kutoka maeneo mbali mbali ya Tanzania sambamba na
kuwashirikishi kikamilifu wamiliki wa ngalawa kutoka maeneo enyeji ya Tumbe,
Shumba mjini, Kiuyu, Msuka, Tondooni na kwengineko ambapo ngalawa kati ya 30
hadi 50 zitashiriki.
Kampuni ya
Rafiki Network imeanzishwa mwaka 2016 na kusajiliwa visiwani Zanzibar ambapo
miongoni mwa kazi zake ni kuandaa matukio mbali mbai ya Elimu na Utamaduni kwa
lengo la kuiwezesha jamii kimaisha kwa kufungua milango ya fursa za ajira
sambamba na kukuza utalii wa ndani na wa nje hapa nchini.
Resi hizi za
Ngalawa ndio tukio la mwanzo kubwa kuandliwa na Kampuni ya Rafiki Network
ambapo wadau mbali mbali kama ZANTEL, TIGO, HALOTEL, ZSSF, Vigor Group of
Companies, TASAKHTA Hospitals na Sun Tours zimeombwa kudhamini tukio hili.
Kampuni nyengine ni Hotel ya Tembo, Serena na nyenginezo ambapo pia mashirika
mbali mbali ya ndege pia yameombwa kutoa
udhamini.
“ Kwa hakika
tuna tamaa kubwa ya kupata mashirikiano na wadhamini wetu. Hadi sasa TASAKHTA
Hospital na Sun Tours wamejitokeza rasmi kudhamini sehemu ya tukio hili. Hata
hivyo tunawakaribisha wadhamini wengine waweze kuiona fursa iliyopo mbele yao
na wajitokeze kudhamini tukio hili lenye manufaa kwao na jamii kwa ujumla.”
Bwana Hamad Omar alitoa wito sambamba na kuushukuru Uongozi wa Hospitali ya
TASAKHTA na Kapmuni nguli ya utalii visiwani Zanzibar ya
SUN Tours kwa kukubali
kushiriki na kudhamini sehemu ya tukio hili.
Tukio
hili sambamba na kudhaminiwa na mashirika mbali mbali linatarajiwa kuhudhuriwa
na vyombo mbali mbali vya habari vya ndani na nje ya nchi ambapo idadi kubwa ya
wageni na washabiki inatarajiwa pia kujitokeza kwa wingi kujionea tukio hili la
kihistoria katika nchi yetu
No comments:
Post a Comment