Wazee wa mabaraza ya shehia ya Wilaya ya
Micheweni ya mfuko wa pensheni
wakishiriki kongamano la siku moja katika shamra shamra za kuazimisha siku ya
wazee duniani zilizofanyika katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari Micheweni
Pemba.
Dkt.
Issa Ahmada Mselem akiwashauri wazazi kutumia huduma za afya kwa mujibu wa
maelekezo ya madaktari na kwenda hospitali kwa mujibu wa ratiba wazipangiwa kuimarisha
afya zao katika kongamano la siku moja la maadhimisho ya siku ya wazee duniani
huko Micheweni Pemba.
Nd
Salmin Sheha Haji Mrajisi wa vizazi na vifo akifungua kongamano la siku moja la
wazee wenye umri wa miaka zaidi ya 70 na kuendelea katika ukumbi wa Shule ya
Sekondari Micheweni tarehe 30/09/2016 wa
mwisho (kulia) ni Afisa wa Pensheni Jamii kutoka Wizara ya kazi Zanzibar.
Mrajisi
wa vizazi na vifo wilaya ya Micheweni akiwasihi wazee wenye umri zaidi ya 70 na
kuendelea kwenda hospitali kupima afya zao na kufuata kanuni za afya bora na
wafahamu kuwa uzee pekee ni ugonja na kuwataka wafanye mazoezi kila siku katika
ukumbi wa Skuli ya Sekondari Micheweni Pemba.
Afisa
kutoka wizara ya kazi akiwatanabahisha viongozi wa mabaraza ya pensheni ya
wilaya ya Micheweni kufikiria afya zao, umoja na maelewano na kuanzisha miradi
midogo midogo itakayowasaidia kupunguza ukali wa umaskini katika kongamano la
siku ya wazee duniani wilayani humo.
Picha zote na Hamad Shapandu Mwinyi, Pemba
No comments:
Post a Comment