Habari za Punde

Mkutano wa uhamasishaji wa kujiunga na kituo cha Elimu Mbadala, Wingwi Pemba

 Baadhi ya Wanafunzi ambao walikosa masomo yao kwa kuacha Skuli kwa sababu mbali ndani ya Wilaya ya Micheweni Pemba, wakishiriki katika mkutano wa uhamasishaji wa kujiunga na kituo cha Elimu Mbadala

kilichopo Wingi Mtemani Wilayani humo ambao ulitayarisha na Idara ya Elimu mbadala na Watu wazima Zanzibar.

 Baadhi ya Wanafunzi ambao waliacha Skuli kwa sababu mbali mbali wakionesha umahiri wao wa kusoma juu ya ubao, huko katika Kituo cha Elimu mbadala kilichopo Wingwi Mtemani Pemba.

 Mratibu wa Idara ya Elimu mbadala na Watu wazima kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya amali Pemba, Hija Hamad Issa, akifunguwa mkutano huo kwa Wanafunzi ambao walihudhuria katika mkutano huo wa uhamasishaji wa kujiunga na Kituo cha Elimu mbadala kilichopo Wingwi Mtemani .


Baadhi ya Wanafunzi ambao waliacha Skuli kwa sababu mbali mbali wakionesha umahiri wao wa kusoma juu ya ubao , huko katika Kituo cha Elimu mbadala kilichopo Wingwi Mtemani Pemba.

 
 Mtowa mada katika mafunzo ya Uhamasishaji wa vijana kujiunga na Vituo vya Elimu mbadala ambae ni Mkuu wa Divisieni ya Elimu mbadala na watu wazima Zanzibar , Halima Tawakal Khairalla, akitowa mada kwa Vijana wa
Wilaya ya Micheweni Pemba, ambao waliacha skuli kwa sababu mbali mbali
Mkurugenzi wa Idara ya Elimu mbadala na Watu wazima Zanzibar, Mashavu Ahmada Fakih, akizungunza na Vijana hao samabamba na kuchangia masuala mbali mbali juu uhamasishaji wa Vijana juu ya kujiunga na kituo cha
elimu mbadala na watu wazima kilichopo Wingwi Wilaya ya Micheweni Pemba.Picha na Habiba Zarali -Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.