Habari za Punde

Serikali Inaleta Maendeleo Bila ya Upendeleo.

Na salmin Juma -Pemba
Naibu waziri wa ujenzi mawasiliano na usafirishaji Mhe.Mohamed Ahmada Salum amesema nia ya Serekali ya Mapindunzi ya Zanzibar chini ya uongozi  mahiri wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein ni kuwapelekea maendeleo wananchi wake bila ya upendeleo wala  kuangalia  itikadi za  wananchi  wake.

Ameyasema hayo wakati wa ziara  zake ya kukagua barabara za ndani ikiwemo  barabara ya  Kichangani  jimbo la  wawi  pamoja  na  barabara  ya Wesha  hadi mkumbuu ilioko jimbo la  ziwani.

Amesema  kuwa  serekali inafahamu kiu ya  wananchi ya kutaka kuwa nahuduma bora za barabara  lakini kutokana na hali ya uchumi barabara hizo zitafanyiwa matengenezo  awamu kwa  awamu.

Aidha  amewataka  wananchi  kuiunga mkono serekali kwa  jitihada kubwa inayofanya kwa wananchi wake ya kutaka  kuwaletea maendeleo  kwa  wananchi wote.

Nae  mwakilishi wa jimbo la Ziwani Suleiman Makame amepogeza  juhudi zinazochukuliwa na Mh Naibu Waziri kwa  kufuatilia kero za  wananchi na  kutafuta njia mbadala zinazoweza  kutatua kero hizo.
Kwa upande wa wananchi wameahidi kutowa ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha lengola serekali lakuwaletea maendeleo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.