Habari za Punde

Naibu Waziri Mhe.Choum Awataka Walimu Kubuni Mbinu Nzuri za Kufundisha - Pemba.

Na Salmin Juma -Pemba
Naibu Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Mhe.Chuom Kombo Khamis, amewataka walimu wa Skuli ya Sekondari Micheweni kuwa wabunifu katika ufundishaji ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi katika skuli hiyo  .

Amesema Taifa linawategemea walimu kuweza kuzalisha wataalamu, na kuwasisitiza kuandaa mikakati itakayofanikisha wanafunzi kusoma kwa bidii na kwa ushidani.

Katika  hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Katibu Tawala Wilaya ya Michweni, Hamad Omar Small wakati akikabidhi vitabu kwa skuli hiyo amesema serikali inawategemea zaidi walimu katika kuwajenga vijana kuwa na  maadili mema.

Amesema  iko  haja kwa Kamati ya Skuli  na Walimu , kuhakikisha wanashirikiana kudhibiti utoro wa wanafunzi pamoja na kuitisha mikutano ya mara kwa mara ya wazazi kujadili maendeleo ya wanafunz katika Skuli hiyo .

Aidha amewataka walimu na wanafunzi kuvitunza vitabu hivyo ili viweze kudumu na kutumika kwa muda mrefu .
Akipokea vitabu hivyo Mwalimu Mkuu wa Skuli hiyo ndg ,Abdalla Hamad ali  amesema vitapunguza tatizo la uhaba wa vitabu na kwamba ameahidi kuvitunza ili lengo lililokusudiwa liweze kufikiwa .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.