Habari za Punde

Wajasiriamali Wakiwa katika Ziara ya Kimasomo ya Kilimo cha Mbogamboga.

Afisa Mdhamini wa Kamiseheni ya Utalii Kisiwani Pemba, Suleiman Amour Suleiman, akizungumza na wajasiriamali mbali mbali kutoka Wilaya ya Micheweni, wakati walipotembelea kujifunza kwa vitendo kilimo cha mboga mboga huko Weni Wilaya ya Wete, wakati wa ziara yao ya Vitendo
Mkulima wa Mboga Mboga kutoka Wilaya ya Wete, aliyejulikana kwa jina la Mohamed akiwaeleza jambo wajasiriamali wa Wilaya ya Micheweni juu ya upandaji wa Kilimo cha Mitungule kinachoendana na soko la kitalii, wakati walipofanya ziara ya kutembelea shamba la Mboga mboga la mjasiriamali huyo
Mjasiriamali wa Kilimo cha Mboga mboga Weni Wilaya ya Wete, aliyejulikana kwa jina la Mohamed akiwaonyesha wajasiriamali kutoka Wilaya ya Micheweni, mbolea anazotumia katika kilimo chake hicho cha mboga mboga.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.