Na Haji Nassor, Pemba
FAMILIA 10 zenye wastani wa watu 60,
wanaolima bonde la Malindi shehia ya Kilindi wilaya ya Chakechake Pemba,
huwenda wakakosa eneo la kilimo cha mpunga, kutokana na mashamba wanayolima,
kuanza kuingia maji ya bahari, kwa watu wasiofahamika kuchota mchanga kwa muda
miaka mitatu sasa.
Kutokana
na kadhia hiyo, tayari wakulima watatu wameshayahama mashamba yao, na wengine
saba hulazimika kufikia mashimo yatokanayo na uchotaji wa mchanga kila mwaka
kabla ya kuanza kilimo hicho, jambo ambalo walisema halileta mavuno mazuri.
Wakizungumza
na mwandishi wa habari hizi, wakulima hao walisema maeneo hayo wanaendesha
kilimo cha mpunga kwa zaidi ya miaka 30, ingawa katika miaka mitatu ya hivi karibuni,
kumejitokeza watu wanaochota mchanga kwa ajili ya biashara.
Walisema
wapo wanachota mchanga kutoka mjini Chakechake na wengine kijijini kwao, hali
ambayo inatishia kukosa kilimo cha mpunga ndani ya bonde hilo, pia kusababisha
uharibifu mkubwa wa mazingira.
Mkulima
Jafar Othman Khamis, alisema wapo wenzao watatu wameshaachana na kilimo hicho,
kutokana na mashamba yao kuvamiwa na maji ya bahari, na kuua mbegu yao ya
mpunga.
“Kwakweli
uchotaji mchanga ndani ya bonde hili la Malindi, umekuwa tatizo, maana maji ya
bahari yanapanda juu, na kuhatarisha kilimo chetu cha mpunga’’, alifafanua.
Nae
Jokha Seif Baki, alisema wameshafuatilia tatizo hilo kwa kamati ya maendeleo ya
kijiji chao bila ya mafanikio, licha kuwepo kwa ushahidi juu ya uchotaji huo
mchanga ndani ya bonde hilo.
“Tokea
siku ya kwanza tulipogundua tatizo hili na kufanya doria, juu ya wizi wa
mchanga ndani ya mashamba yetu, tulisambaaza taarifa kwa wanakijiji wenzetu,
lakini walipuuza’’,alifafanua.
Kwa
upande wao wakulima Ali Othman Khamis na Asaa Ali Omar, walisema baada ya kuona
hali hiyo imekithiri, walitoa taarifa kwa uongozi wa shehia ili kudhibiti hali
hiyo.
“Lakini
sheha hakuonekana kulichukulia hatua za haraka tatizo letu, sasa sijua kwa
sababu za kisiasa au wanaochota mchanga ni watu wake’’,walisema.
Sheha
wa shehia ya Kilindi wilaya ya Chakechake Abuu Abrahaman Salim, alikiri kuwepo
kwa kadhia hiyo, na amesema amechachukua hatua ya kupinga marufuku.
“Ni
kweli wakulima hao walinifika na kunielezea tatizo la uchukuaji mchanga ndani
ya mashamba yao, lakini nimeshapiga marufuku na wakimkamata anaechukua mchanga
waniletee’’,alifafanua.
Hata
hivyo sheha huyo alisema, lazima wananchi wajenge utamaduni wa kuyalinda maeneo
yao na uharibifu na uchafuzi wa mazingira, unaofanywa.
Shehia
ya Kilindi wilaya ya Chakechake, pamoja na kuwepo kwa tatizo la uchimbaji
mchanga kiholela, lakini katika za hivi karibuni, kumeibuka ukataji miti kwa
kasi kwa kutumia msumeno wa moto ‘chensoo’.
No comments:
Post a Comment