Na Mwashamba Juma.
WAJUMBE wa
Bunge la Afrika Mashariki (EALA) wamesema tatizo la fedha linaloikabili Jumuiya
ya Afrika Mashariki (EAC) sio suala la serikali moja moja bali ni la nchi
wanachama wote.
Walisema
changamoto hiyo imekuwa sugu na ya muda mrefu, hali waliyoielezea kuchangia
kuteteresha uchumi wa jumuiya hiyo na kusababisha kusimama kwa baadihi ya kazi
za jumuiya.
Wakijadili
hoja ya pamoja kwenye kikao cha tano cha mkutano wa pili wa bunge la tatu la
EALA, huko ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani mjini Unguja, hoja
iliyowataka wajumbe hao kuwa na njia mbadala ya kuichangia EAC kutokana na
uhaba wa fedha unao ikabili jumuiya hiyo.
Wajumbe hao
wa bunge la EALA walishauriana kusimama pamoja na kutumia sauti ya moja ili kukabiliana
na changamoto zilizopo mbele yao.
Akichangia
hoja iiliyowasilishwa bungeni hapo kwakuzungumia mbinu mbadala walizojadiliana
kutatua changamoto hiyo, Mbunge wa Afrika Mashariki anaeiwakilisha Tanzania
kwenye jumuiya hiyo, Mhe. Maryam Ussi Yahya alisema licha ya changamoto za
kiuchumi zinazoikabili EAC anaamini bado itaendelea kusongambele katika
kuyafikia malengo iliyojiwekea.
Alieleza
suluhu ya kuondosha tatizo liliopo sio suala la siku moja bali linahitaji mda
hadi hali kutengemaa.
Alisema
asilimia kubwa ya mapato ya jumuiya hutegemea ufadhali kutoka Jumuiya za
kimataifa, hali iliyochangia kukwamisha kwa baadhi ya shughuli za EAC.
"Si
kama tunataka jumuiya iendelee kutegemea wafadhili kutoka nje, tunachotaka nchi
wanachama tuchangie asilimia mia moja kwaajili ya kuiinua jumuiya yetu"
alieleza Mhe. Yahya.
Alisema wajumbe
wanamatumaini makubwa kuwa jumuiya itazidi kusongambele licha ya kukabiliwa na
changamoto za fedha zilizosababisha kuzorotesha kwa baadhi ya kazi za jumuiya
hiyo.
Nae Mbunge
kutoka Jamuhuri ya Kenya, Peter Mathuki alieleza mjadala uliopo mbele yao ni
muhimu kwani unajadili hatima ya wanachi wa mataifa matano ya Afrika Mashariki,
hivyo azitaka nchi wanachama za EAC kutumia maliasili zao kwa ufanisi sambamba
na kutekeleza miradi yao ya maendeleo kwa kuhakikisha inaiongezea mapato
jumuiya ili kupunguza tatizo la uhaba wa fedha linaloikabili jumuiya hiyo.
Akizungumzia
suala la ushirikiano kwa nchi wanachama wa EAC katika kukabiliana na changamoto
ya fedha inayowakabili, Mbunge kutoka Uganda, Dora Byamukama alilisitiza
kufanyakazi pamoja kwa sauti moja kwaajili ya kuiendeleza EAC ya sasa na baadae
ili isitetereke kwa changamoto za kiuchumi.
Kwa upande
wake Martin Ngoga, Mbunge kutoka Rwanda wakati akichangia hoja hiyo bungeni
hapo, alieleza wajibu wao kama nchi wanachama kuangalia mbinu mbadala za
kudhibiti hali ya fedha ya jumuiya yao isidhorote.
Akizungumzia
juhudi za haraka zilizochukuliwa na Jumuiya hiyo ili kuiokoa kutoka kwenye hali
mbaya ya mgogoro wa fedha unaoikabili, Katibu mkuu wa Jumuiya hiyo ambae pia ni
Mbunge anaeiwakilisha Burundi katika bunge la EALA, Mhe. Libera Mfumukeko
alisema EAC imefanikiwa kukusanya kiasi cha dola milioni tano kutoka kwa nchini
wanachama wake.
"Wiki
mbili zilizopita, Jumuiya yetu ya EAC imepokea dola milioni tano kutoka kwa wanachama
wake ikwemo Burundi iliyochangia dola milioni 2. 8" alieleza.
Alizitaja
nchi nyengine zilizochangia kiasi hicho cha fedha ni pamoja na Kenya dola
milioni mbili na mwenyeji Tanzania dola milioni moja na kuongeza kuwa nchi za
Rwanda na Uganda wanategemea kuchangia siku za karibuni.
Mfumukeko ambae
pia ni mhasibu mkuu wa EAC alieleza kwasasa hali ya fedha kwa jumuiya hiyo kidogo
inaridhisha ambayo inaweza kuisukuma walao kukidhi mahitaji yake ya lazima.
Sambamba na
kueleza kuwa EAC bado inapambana kufanikisha juhudi zaidi sio kwa kupata
misaada kutoka kwa wafadhili na wadau wa maendeleo pekee, hata kwa juhudi za
wakuu wa nchi wanachama wa jumuiya wakiwemo maraisi wa nchi tano zinazounda
jumuiya hiyo ya EAC.
Akizungumzia
michango ya wadau wao wa maendeleo kwenye jumuiya hiyo, Mfumukeko alieleza
awali walichelewa kuchangia ndio maana EAC ilitetereka kifedha nakuongeza kuwa siku
chache baada ya kikao hicho cha tano cha bunge la tatu la mkutano wa pili wa
EALA kuna baadhi yao walijitokeza kuichangia EAC, wakiwemo Wajurumani, Norway
na Denmark.
Pia alieleza
kuwa EAC walisaini mkataba wa Euro milioni 85 kutoka kwa Umoja wa Ulaya (EU) na
kueleza kiasi hicho cha fedha kitakachoingia kitasukuma miradi mingi ya
maendeleo ambauo EAC imejipangia kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Aliongeza
kuwa EAC pia imesaini na shirika la kimataifa la (US aids) mkataba wa dola
milioni 50.
Hata hivyo
alieleza uhusiano wa EAC na wadau wake wa maendeleo bado unaendelea vyema licha
ya kuwepo kwa baadhi ya changamoto zilizochelesha kuchangiwa fedha mapema
miongoni mwao alizieleza ni pamoja na migogro ya ndani ya EU ikiwemo Kujitoa
kwa Uingereza na ongezeko la wakimbizi kwenye nchi za Ulaya limeicheleweshea
EAC kupokea misaada kutoka kwa jumuiya hiyo.
Mapema
akiwasilisha hoja hiyo ya pamoja iliyowataka wajumbe wa bunge la EALA kutafuta
mbinu mbadala za kuichangia jumuiya ya EAC kutokana na uhaba wa fedha
unaoikabili, Mbunge kutoka Kenya Judith Pareno alieleza migogoro ya fedha
inayoikabili EAC imekuwa mikwazo cha kusumuma mbele miradi ya maendeleo na
uchumi wa jumuiya hiyo kwa nchi wanachama wake.
Mkutano wa
pili wa bunge la tatu la EALA pia uliwasilisha mswada wa " Kudhibiti
usafirishwaji wa binaadamu katika nchi za Afrika Mashariki" ambao
liwasilishwa na Mhe. Maryam Ussi Yahya, Mbunge wa Afrika Mashariki
anaeiwakilisha Tanzania.
Aidha spika
wa bunge hilo la EALA, Mhe. Daniel Kidega alikighairisha kikao hicho hadi
Oktoba 18 mwaka huu kwaajili ya kuujadili mswada wa " Kudhibiti
usafirishwaji wa binaadamu katika nchi za Afrika Mashariki".
No comments:
Post a Comment