Habari za Punde

Afariki Baharini akivua

Na Salmin Juma kutoka Pemba

MZEE  mmoja anayejulikana kwa jina la Saleh Ali Mbwana mwenye umri wa miaka 45 mkaazi wa Maziwang’ombe Wilaya ya Micheweni  amefariki dunia baada ya kuzama   baharini akiwa katika shughuli zake za  uvuvi .

Akithibitisha kutokea kwa tokeo hilo kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Kamishna Msaidizi Haji Khamis Haji  amesema tukio hilo limetokea oktoba 20  mwaka huu majira ya saa saba za mchana katika bahari ya Maziwang’ombe .

Amesema kwamba kabla ya kifo chake , marehemu aliondoka nyumbani kwake kwenda baharini kuvua , na alifikutwa na mauti hayo katika bahari  wakati akitekeleza shughuli zake za uvuvi.

Kufuatia kutokea kwa tukio hilo Kamanda Haji  amewataka wananchi hususani wanaotoka maeneo ya ukanda wa bahari wanapokwenda kuvua au kulima mwani  kufuatana na wenzao ili patakapo tokea hitilafu waweze kusaidiana

Akizungumza baada ya uchunguzi daktari dhamana wa hospitali ya Wilaya ya Micheweni Dk  Rashid Daudi Mkasha amesema chanzo cha kifo chake kimesababishwa na kukosa hewa  baada ya kukaa chini ya maji ya  bahari kwa muda mrefu .

Mwili wa marehemu umekabidhiwa kwa ndugu na jamaa baada ya kufanyiwa uchunguzi na dk wa Serikali ambapo mazishi yake yalifanyika katika maburi ya Maziwang’ombe

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.